Header Ads Widget

MMOJA AUAWA, WANNE WAJERUHIWA KWA KUKATWA MAPANGA HANDENI TANGAMtu mmoja ameuawa huku wengine wanne akiwemo mtoto wakijeruhiwa wilayani Handeni mkoani Tanga baada ya kukatwa mapanga huku wananchi wakijawa na hofu kuhusiana na tukio hilo.

Tukio hilo limetokea katika kitongoji cha Kwamagome kilichopo ndani ya halmashauri ya mji Handeni majira ya saa kumi na mbili jioni,huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda akithibisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo.