Header Ads Widget

ALIYEKUWA MBUNGE JIMBO LA MBOGWE ASHINDWA KUTETEA NAFASI KURA ZA MAONI

Katibu wa CCM wilaya ya Mbogwe Bi Grace Shindika akionyesha mojawapo ya kura zilizopigwa kabla  ya kuanza kuhesabiwa.

Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Mbogwe Mkoani Geita Augustino Manyanda Masele ameshindwa kutetea nafasi yake katika kura za Maoni ambapo Bw Nicodemas Maganga amemshinda kwa kupata Kura 265 dhidi ya 212 alizopata Masele huku mshindi wa tatu akipata kura 16. 

Akitangaza Matokeo ya Uchaguzi huo Msimamzi wa Uchaguzi Jimbo la Mbogwe ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita Bw David Azalia amesema kuwa zoezi hilo limekuwa huru na haki ambapo kila mpiga kura ameshuhudia zoezi hilo wakati kura zikihesabiwa na kumtangaza Bw Nicodemas Maganga kuwa Mshindi wa Kura hizo. 

Awali akizungumza kabla ya kuanza kwa zoezi la kupiga kura Katibu wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbogwe Grace Shindika amewaambia wajumbe kuwa kura hizo si kielelezo cha ushindi kwa Mgombea bali ni hatua ya awali ya kumpata Mgombea atakeyepeperusha Bendera ya chama hicho, ambapo amesema kuwa mara baada ya hapo majina yatawasilishwa kwenye kamati ya siasa ya Mkoa kisha kamati  Kuu ya taifa. 

Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbogwe Bw Christopher bahari aliwataka wagombea kuchagua viongozi watakaoenenda na kasi ya Rais wa awamu ya Tano Dr John Magufuli sambamba na kuchagua kiongozi atakayebadili na kuletamabadiliko kwa jamii ikiwa ni pamoja na kutatua kero za wananchi

Bahari amesema kuwa nchi kwa sasa imeingia katika uchumi wa kati wa kati hivyo wanatakiwa viongozi watakaohakikisha wanapiginia maslahi ya Umma ikiwemo kusimamia miradi ya maendeleo pamoja na fedha zinazotolewa na serikali.

“niwaombe katika uchaguzi huu tuhakikishe tunachagua viongozi amabao watalaeta tija na masalahi ya umma,taifa na jamii kwani mkileta viongozi ambao ninyi mmewapanga kwa kitu kidogo haitakusaidieni  tuleteeni viongozi watakaoinua uchumi na kutatua kero za  zenu”

Aidha  baada ya kutangazwa  kwa kura za maoni Masele ameshindwa na Bw Nicodemas kwa Kura 265 kwa 212 ambapo akizungumzia  matokeo hayo aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Augustino Masele amesema kuwa amepokea kwa furaha matokeo hayo na kusema kuwa ataendelea kushirikiana na Mgombea aliyepita

Masele amesema kutokana na demokrasia ndania ya chama hicho umesaidia zoezi kuwa huru na kupelekea ushindi kupatikana kwa mpinzani wake wa karibu

Naye Mgombea aliyepita katika kura hizo Nicodemas Maganga amewashukuru wajumbe  wote wa Mkutano mkuu wa wilaya  kwa kumuamini na kumpitisha kwa kura nyingi ambapo amehaidi kushirikiana na Wananchi wote wa wialya hiyo katika kuleta maendeleo ya jamii na umma

Maganga ameongeza kuwa mara baada ya jina lake kurudi kutoka kamati kuu ya Chama taifa atahakikisha  anashirikiana na wananchi wote wa jimbo hilo pamoja na kuondoa changamoto zinazoikabili jamii hiyo ikiwemo migogoro ya ardhi, changamoto ya  Maji, na huduma za afya.

Jumla ya Wagombea 31 walijitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ambapo jumla ya Wagombea 29 walijitokeza  huku wawili wakitokomea kusikojulikana kati yao mwanamke akiwa mmoja tu huku jumla ya wajumbe waliotakiwa kupiga wakiwa mia zaidi ya 600 ambapo waliopiga kura walikuwa 584 moja ikiharibika Nicodemas Maganga akiongoza kwa kura 265  nafasi ya Pili ikiongozwa na Augustino Masele
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbogwe ambaye ni Katibu wa Itikadi na uenezi Mkoa wa Geita David Azalia  akitoa maelekezo kwa Wajumbe na wagombea wa Mkutano mkuu wa Jimbo hilo.
Katibu tawala wa Wilaya ya Mbogwe Bw Christopher Bahari akisisitiza juu ya upatikanaji wa viongozi bora na si Bora kiongozi.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Augustino Manyanda  Masele Akinadi na kuomba kura kwa Wajumbe wa Mkutano  mkuu wa CCM  katika Jimbo hilo.
Mshindi wa Kura za Maoni za  mgombea wa Nafasi ya Ubunge jimbo la Mbogwe Bw Nicodemas Maganga mapema akiomba kura  kwa wajumbe wa mkutano mkuu.
Uhakiki wa Karatasi za kupigia kura kabla ya zoezi la upigaji kura kuanza 
 Wagombea wa nafasi ya Ubunge jimbo la Mbogwe wakiomba Mungu Kabla ya kuanza kwa Mchakato wa Kupiga kura.
 Wajumbe wakiendelea kufuatilia kujinadi kwa wagombea.
 Mmoja wa Wagombea wanawake pekee ambaye amejitokeza kati ya wagombea 31 ambapo ameonyesha ujasiri kuwakabili wanaume 30.
 Tazama picha mbalimbali chini 











 






@ShinyangaPressClub Jukwaa la Habari Tanzania 
 Uhakika wa Taarifa.
#Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 789 632 732, +255 756 546 015 au +255 686 057 440 Email : shinyapress@gmail.com