Header Ads Widget

JPM AMTUMBUA KAFULILA, DC MASWA AWA RAS SONGWE, WAZIRI MKUCHIKA NAE ATEUA



David Kafulila

MASAA kadhaa baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kufanya uteuzi mbalimbali wa wakuu wa wilaya, makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu wa wizara mbalimbali leo asubuhi, Jioni hii amefanya uteuzi mwingine wa wakuu wa wilaya, makatibu tawala na wakurugenzi.

Katika uteuzi huo, aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, David Kafulila ameondolewa kwenye nafasi hiyo, na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Dkt. Seif Shekhilage.

Vile Vile, Mussa Ramadhan Chogelo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, huku Aswege Enock Kaminyonge akiteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Maswa.

Soma zaidi taarifa ya uteuzi huo hapa chini, iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa leo Julai 17, 2020.