Header Ads Widget

BERNARD MORRISON WA YANGA AKAMATWA, AACHIWA KWA DHAMANA


Bernard Morrison

MATUKIO ya utata na utovu wa nidhamu yanazidi kumuandama mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison baada ya kukamatwa na askari polisi kisha kuachiwa baadaye.

Tukio hilo linadaiwa kutokea mchana huu Alhamisi Julai 30, 2020 baada ya askari wa doria waliolitilia shaka gari la mchezaji huyo kisha kutaka kulipekua sehemu iliyokuwa limeegeshwa na Morrison kugoma na kusababishwa kupelekewa na wenzake polisi.


"Askari walihisi harufu ya kitu kutoka ndani ya hiyo gari sasa walipotaka kumfanyia upekuzi akagomea upekuzi huku akileta utata akitaka kuwarekodi polisi," kilisimulia chanzo hicho na kuongeza; 
"Baadaye polisi walifanikiwa kumtaka waelekee kituo cha polisi kwa hatua zaidi akakubali na akatoa maelezo yake pale kituo cha Polisi Oysterbay." Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Edward Bukombe ambaye alithibitisha kushikiliwa kwa muda kwa mshambuliaji huyo raia wa Ghana.