Header Ads Widget

ALIYESOMESHWA NA MKAPA HADI CHUO KIKUU AFUNGUKA

 Hayati Benjamin William Mkapa

SUNDAY Abdul, mmoja wa wananchi aliyesomeshwa na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, Sanday Abdul, ameeleza alivyoweza kufikia elimu yake kufika chuo kikuu kwa kusomeshwa na Rais Benjamin Mkapa, akilipiwa gharama zote za masomo.

Akizungumza na Nipashe wakati wa Maziko ya kiongozi huyo aliyefariki usiku a kuamkia Julai 24, mwaka huu, alisema walikuwa wanafunzi 12 waliofahulu katika shule msingi Lupaso ambako Mkapa alisoma na kuahidi kuwasomesha hadi atakaposhindwa wao.

“Pamoja na kutulipia ada, lakini alitulipia gharama zote za mahitaji muhimu ya maisha kama chakula, mavazi alitugharamia, na nauli ya kwenda na kurudi kijijini kila shule na vyuo vikufunguliwa na kufungwa, na aliwanunulia vitabu alivyoona vitawasaidia kwenye masomo yao,”alisema.
 
Abdul alisema alimaliza Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), mwaka 2015 na kupata Shahada ya Ualimu na kwamba kwangu ni baba, kiongozi na mlezi kwa kuwa bila yeyea asingeweza kusoma.

Alikuwa anapenda elimu, aliniambia utasoma hadi pale utakapoacha kusoma, tulimaliza wote hatukumwangusha na wote tunafanya kazi sehemu mbalimbali. Pia kamsomesha mdogo wake.

Alisema alipata taarifa za msiba ikiwa ni siku chache akiwa ametoa kijijini, mdogo wangu aliingia mtandaoni na kunieleza Mzee amefariki nikahakikisha kwa kuingia mtandaoni niliona kwenye vyombo vya habari, nilikuwa Dar es Salaam naelekea Moshi ninapoishi, ikabidi nigeuze nirudi.

Alisema watu walimtegea sana na kwa sasa wanaona mambo mengi yatakwama kwa kuwa alikua na miradi mingi ikiwamo kuanzisha chuo cha Nesi, na kuimba serikali kusaidia miradi hiyo ikamilike.