Header Ads Widget

15 WADAKWA KATAVI KWA KUMUOZESHA MWANAFUNZI WA DARASA LA 5


Jeshi la Polisi limewakamata Watuhumiwa 15 wakiwemo Wazazi 2 kwa kumuozesha Mwananfunzi wa darasa la 5 kwa mahari ya ng'ombe 12.
 
Kamanda wa Polisi wa Mkoani humo, Benjamin Kuzaga amesema wamefanikisha kuisambaratisha ndoa hiyo ya kimila na wanaendelea na juhudi za kumtafuta muoaji ambaye alitoroka

Ndoa za Utotoni, chini ya miaka 18 (Wavulana na Wasichana) ni marufuku Tanzania kutokana na kushinda kwa kesi iliyofunguliwa mwaka 2016 na Mkurugenzi wa Asasi ya Kiraia ya Msichana Initiative, Rebecca Gyumi. Awali umri wa kufunga ndoa ulitofautiana kwa Wavulana na Wasichana.

Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, Kifungu cha 148 (1&2) kinasema Mtu yeyote anayefunga ndoa huku akijua au akiwa na sababu ya kujua kuwa mwenza wake yupo chini ya umri wa ndoa atahukumiwa kifungo cha miaka 3.

Pia, mtu yeyote anayakeshiriki katika ndoa hiyo atakuwa na kosa na atahukumiwa kifungo kisichozidi miaka miwili.