Header Ads Widget

WAGANGA TIBA ZA ASILI WAIOMBA SERIKALI KUFUNGUA KITUO MAALUM CHA KUTAMBUA UBORA WA DAWA ZAO




Mwenyekiti wa Shirika lisilo la kiserikali (Kigwa) mkoani Shinyanga Christopher Ipuli akikabidhi balakoa kwa mwenyekiti wa Umoja wa waganga wa tiba asili manispaa ya Shinyanga Kassim Kuhangaika jana kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa virusi vya Corona zilizotolewa na Shirika hilo. 

Na Suzy Luhende - Shinyanga Press Club Blog
Umoja wa waganga wa tiba asili manispaa ya Shinyanga mkoani hapa, umeiomba serikali ifungue kituo kwa ajili ya kupima dawa wanazotengeneza ikiwa ni pamoja na kuwapatia ardhi kwa ajili ya kupanda miti ambayo hutumika kwa dawa mbadala kwa matumizi ya binadamu. 

Licha ya kuomba kituo pia wameiomba serikali kuwapatia mashine ya kuchakata na kusaga mizizi na magome ya miti ambayo inatumika kutengenezea dawa ya binadamu 

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa Umoja wa waganga wa tiba asili manispaa ya Shinyanga Kassim Kuhangaika wakati akipokea barakoa 52 kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali ( kikundi Cha wataalamu wa afya (KIGWA) mkoani Shinyanga, Christopher Ipuli.

Kuhangaika alisema kwa sababu serikali haitaki lamri chonganishi ambazo zinasababisha vifo na uchonganishi na wao wanauza dawa na kutoa maelekezo, ni vizuri sasa serikali ikafungua kituo cha kupima dawa zao, na waganga wengine walioko vijijini waweze kufika na kupata elimu ili wasiendelee na lamri chonganishi.
Mwenyekiti wa Umoja wa waganga watiba asili manispaa ya Shinyanga Kassim Kuhangaika akishukuru baada ya kukabidhiwa balakoa na mkurugenzi kikundi binafsi cha wataalamu wa afya (KIGWA) mkoa wa Shinyanga, Christopher Ipuli.

Mmoja wa wauzaji wa dawa za asili katika eneo la Stendi ya Zamani katika manispaa ya Shinyanga, Hassan Kharim amesema miti inavunwa sana katika nyakati hizi hivyo wanaweza wakajikuta wanakosa dawa, Ni vizuri serikali ikawapatia maeneo ili waweze kupanda ziendelee kuwepo vizazi na vizazi.

Naye Steven Philipo muuzaji wa dawa za asili katika manispaa ya Shinyanga, ameishukuru serikali kwa kuiona sekta hiyo kwamba inaweza kutibu magonjwa mbalimbali, lakini kuna changamoto ya miti mingi kukatwa maeneo mbalimbali, na wanaitegemea sana kwa ajili ya dawa, lakini wakipatiwa maeneo wakawa wanapanda itasaidia kwa baadae.
Steven Philipo muuza dawa za asili katika stendi ya zamani ya manispaa ya Shinyanga akizungumza baada ya kukabidhiwa barakoa. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisililo la kiserikali (Kigwa) mkoani Shinyanga, Christopher Ipuli ameiomba serikali ifungue kituo kingine cha kupima dawa za asili katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ambayo itapima na kufanya utafiti iweze kusaidia watu wengi. 

"Shirika letu letu lisilo la kiserikali (Kigwa) limeona mnatekeleza wajibu wenu chini ya sheria namba 23 ya mwaka 2002 ikaona iwape balakoa zinazokubalika ili muweze kujikinga na virusi vya ugonjwa wa Corona kwa sababu mnakutana na watu mbalimbali katika kazi zenu, na nyinyi ni mfano wa waganga wengine ambao hawapigi lamri," amesema Ipuli. 
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali (Kigwa) Christopher Ipuli akizungumza na wauza dawa za asili za binadamu katika maeneo ya Stendi manispaa ya Shinyanga mkoani hapa kabla ya kuwakabidhi balakoa kwa ajili ya kujikinga na virusi vya corona.