Header Ads Widget

NITAILINDA KATIBA YA BURUNDI, ASEMA RAIS MPYA WA NCHI HIYO ALIYEAPISHWA LEO

 CHANZO-BBC



















Rais mpya wa Burundi Evariste Ndayashimiye na mkewe

Burundi imemuapisha rais mpya wa taifa hilo , Evariste Ndayishimiye, katika hafla iliofanyika mbele ya raia wa taifa hilo na baadhi ya viongozi kutoka mataifa tofauti.

Katika kiapo chake rais huyo ameapa kulinda katiba ya Burundi, kuheshimu umoja wa raia wa taifa hilo, kutoa haki kwa wote mbali na kutetea mipaka ya taifa hilo.

Kiapo hicho kinatokana na kifungu cha 107 cha katiba ya nchi hiyo

Ikulu ya Rais wa Burundi

Sherehe hiyo iliofanyika katika uwanja wa kandanda wa Ingoma katika mkoa wa Gitega imefanyika wakati ambapo taifa hilo limeathirika na mlipuko wa virusi vya corona.

Rais Evariste baada ya kumaliza kula kiapo alikagua gwaride la kijeshi na baadaye kutoa hotuba .

Muda mchache kabla ya kula kiapo rais Evariste aliombewa na baadhi ya maaskofu ambao walimtaka kufungua milango ya uhusiano mwema na mataifa mengine.

Mbali na kwamba baadhi ya wageni hawakuvalia barakoa, raia wengi waliohudhuria hafla hiyo hawakuvaa kifaa hicho cha kuwalinda dhidi ya corona.

Hatahivyo shirika la msalaba mwekundu liliandaa maji na sabuni kwa raia wote waliokuwa wakiingia katika uwanja huo kuosha mikono yao.
Maelfu ya raia wa Burundi wamefurika katika uwanja huo wakisubiri kuapishwa kwa rais huyo kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa taifa hilo Pierre Nkurunziza. Rais wa Burundi,Makamu wa rais wa Tanzania bi Samia Suluhu na aliyekuwa rais wa taifa hilo Jakaya Mrisho Kikwete
 wamehudhuria katika hafla hiyo ya kihistoria.

Ni matokekeao ambayo yalikuwa yanatarajiwa. Tume ya uchaguzi hii leo imemtangaza Meja Jenerali mstaafu Evariste Ndayishimiye kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika juma lililopita.

Evariste atachukua nafasi ya Rais Pierre Nkurunziza mbaye ameliongoza taifa hilo la Afrika Mashariki kwa miaka 15.

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza Ndayishimiye ni nani? mwanasiasa huyo ni mtu wa karibu wa Nkurunziza na amekuwa Katibu Mkuu wa Chama tawala CNDD-FDD tangu mwaka 2016.

Alizaliwa mwaka wa 1968 katika mkoa wa Gitega, eneo la kati mwa taifa hilo.

Uhusiano wa Ndayishimiye na CNDD-FDD

Bwana Ndayishimiye ni miongoni mwa waliokuwa waasi wa CNDD-FDD waliojiunga na kundi hilo baada ya kunusurika katika mauaji ya kikabila ya wanafunzi Wahutu katika chuo kikuu cha Burundi mwaka 1995, kufuatia mauaji ya rais Melchior Ndadaye mnamo mwaka wa 1993.

Baadae kundi la CNDD-FDD lilibadilishwa na kuwa chama cha kisiasa ambacho kilianza kushiriki katika mazungmzo ya amani mjini Arusha Tanzania mwaka wa 2000 na kuafikiana kuhusu usitishwaji wa vita.

Wakati kundi la waasi la CNDD-FDD lilipojiunga na serikali mwaka wa 2003, Ndayishimiye tayari alikuwa amepandishwa cheo cha Meja Jenerali, na alihamishwa aende kuhudumu katika makao makuu ya jeshi la taifa.


                                   CHANZO-BBC