Mkuu wa wilaya ya
Mbogwe mkoa wa Geita , Martha Mkupasi akizungumza baada ya kupokea mradi wa Badirisha Tabia epuka Covid-19 toka
shirika la SHDEPHA+Kahama utakao toa elimu kwa jamii vijijini kwa miezi mitatu
Na Patrick Mabula , Mbogwe.
Shirika lisilokuwa la Kiserikali la SHDEPHA+ linalotekeleza
mradi wa badilisha tabia epuka Covid-19 wilaya ya Mbogwe mkoa wa Geita limetoa
wito kwa jamii kuishi kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Serikali na
watalaamu wa afya ili kuepukana na maabukizi ya ugonjwa wa Corona.
Akitambulisha mradi huo kwa Mkuu wa wilaya ya Mbogwe meneja
mradi wa shirika la SHDEPHA+ , Martini Nyakitina amesema mradi huo wa miezi
mitatu utakuwa ukitoa elimu kwa jamii inayoishi mjini na vijijini
katika kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na ugonjwa wa Corona.
Nyakitina amesema katika mradi huo wakati wa kutoa elimu
watashirikiana na wahudumu wa afya na vikundi katika kutoa elimu kwenye jamii
kuhusu kujikinga na maabukizi ya virusi vya Covid-19 itakayowasaidia siku zote
kuishi kwa tahadhali siku zote.
Akipokea mradi huo wenye thamani ya Shilingi milioni 30 , mkuu
wa wilaya ya Mbongwe , Martha Mkupasi amesema kwenye jamii bado kunachangamoto
katika kujikinga na maabukizi ya virusi vya Covid- 19 vya homa kali ya mapafu Corona
hivyo elimu hiyo itawasaidia kujikinga na ugonjwa huo.
Mkuu wa wilaya amelishukuru shirika la SHDEPHA+ kwa mradi huo
kwani pia limetoa msaada wa ndoo za maji
pamoja na vitakasa mikono vitakavyopelekwa kwenye mikusanyiko ya watu
katika minada na magulio.
Mkuu wa wilaya ya
Mbogwe mkoa wa Geita Martha Mkupasi akipokea msaada wa ndoo za maji pamoja na
vitakasa mikono kutoka kwa meneja mradi wa Badilisha tabia epuka
Covid_19 Martini Nyakitina wa shirika la SHDEPHA+ , Kahama utakaotoa
elimu kwa wananchi vijijini kuishi kwa tahadhali na kujikinga na ugonjwa wa
Corona.