Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dr Festo Dugange
Na Mwandishi wetu Simiyu.
Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii Wapatao 72, Kutoka Wilayani Itilima Mkoani Simiyu, wamepewa
mafunzo ya kukabilina na Ugonjwa wa Covid 19, unaosababishwa na Virusi Vya
Corona, huku wakiombwa kuwa mstari wa mbele kuisaidia Serikali
katika Mapambano ya kudhibiti Ugonjwa huo ambao umekuwa janga la Dunia
.
Akifungua mafunzo
hayo yaliandaliwa na Shirika la Doctors With Africa /CUAMM kupitia mradi wa
Test and Treat Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dk Festo Dugange amesema
kuwa wahudumu wa afya ngazi ya Jamii wanaoa
wajibu mkubwa wa kuielimisha jamii katika masuala mbalimbali ikiwemo kuchukua
tahadhari ya ugonjwa wa Covid 19.
Dr Dugange amesema ni muhimu wahudumu ngazi ya
jamii kusaidiana na Serikali katika mapambano ya kudhibiti Corona, kwani wahudumu
hao ndio wanaishi karibu na wananchi Maneneo ya vijijini na mijini hivyo ni
vema mafunzo wanayoyapata yakatumika kwa tija na faida kwa jamii inayowazunguka.
“Jamani nyie
wahudumu wa afya ngazi ya jamii ndio mnaishi karibu na wananchi. hapa
leo mnapewa mafunzo na Shirika la CUAMM, haya mafunzo ni muhimu kwa jamii mnayoishi
nayo, Naomba mkayatumie vizuri kuhakikisha mnaisaidia serikali na Jamii kukabiliana
na ugonjwa wa Covid 19,”amesema Dk.
Dugange
Kwa upande
wake Mratibu wa Shughuli za
Kijaamii kupitia Mradi wa Test and Treat kutoka Shirika la Doctors With Africa/
CUAMM, Gasaya Msira amesema lengo lao ni kushirikiana na Serikali
katika mapambano mbalimbali ambapo hufanya shughuli katika Mkoa miwili ya Simiyu na Shinyanga ambapo Shinyanga
zinafanyika katika Wilaya za Shinyanga Manispaa,Shinyanga Vijijini na
Mkoa wa Simiyu zikifanyika Wilaya za Bariadi Mjini na Vijijini .
“Kwa kuwa tunafanya
kazi na Serikali tumeona ipo haja kushirikina na Serikali katika mapambano
dhidi ya Corona kwa kutoa elimu kwa wadumumu wa afya ngazi ya jamii, hawa
wahudumu wataisaidia Serikali kutoa elimu katika jamii inayowazungunga
na jinsi ya kukabilina na ugonjwa huo.”amesema Msira
Msira amesema mpaka
sasa wametoa mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii 72 katika
Wilaya ya Itilima, ambapo hata hivyo watatoa mafunzo baadaye kwa wahudumu 55 wa
Wilaya ya Bariadi Mjini, 49 Bariadi Vijijini huku tayari wakiwa
wametoa Mafunzo kama hayo kwa Mkoa wa Shinganya ambapo Wilaya ya
Shinyanga Mjini na Vjijini wahudumu 109 kwa pamoja wamepata mafunzo hayo.
Awali akizungumza na wahudumu hao wa afya ngazi ya
jamii Mkoa wa Simiyu, Meneja miradi
anayeondoka Bi Veronica Censi amewashukuru
wahudumu hao, kwa kufanya kazi pamoja katika kipindi chake chote
alichokuwa Mtawala na kwamba anajivunia ushirikiano aliyokuwa
akiupata toka kwao.
“Naomba umie fulsa
hii kuwashukuru wote, tumefanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano mkubwa.
Najivunia kwa kiasi kikubwa kuwa nanyi hapa Simiyu. Nitawakumbuka na
nitaendelea kuwa pamoja nanyi asanteni
sana nawashukuru,”amesema Censi
Shirika la Doctors
with Africa/CUAMM limekuwa miongoni mwa Mashirika yasiyo ya Kiserikali
yanayoiunga mkono Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania katika masuala na
Nyanja tofauti tofauti ikiwemo sekta ya Afya,Elimu na Maji.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dr Festo Dugange akisisitiza jambo wa Washiriki wa Mafunzo hayo Mjini Bariadi.
Meneja Miradi wa Shirika la Doctors with Africa/CUAMM Bi Veronica Censi anayemaliza muda wake akiwaaga na kuwashukuru washirika hao kwa muda wote aliofanya nao kazi.

Mratibu wa Shughuli za Kijaamii kupitia Mradi wa Test and Treat kutoka Shirika la Doctors With Africa/ CUAMM, Gasaya Msira akiwaasa wanajamii hao kwenda kutekeleza elimu waliyoipata kwa vitendo.
Kushoto ni Meneja Miradi wa CUAMM Anayeondoka Bi Veronica Censi na anayefuata ni Mganga mkuu wa mkoa wa Simiyu Dr Festo Dugange.
washiriki wa mafunzo ya ngazi ya jamii wakiendelea na Mafunzo
Mmoja wa Washiriki akifuatilia hatua kwa hataua ya elimu wanayopewa
Mtalaam wa Masuala ya Jamii toka CUAMM akiendelea kutoa elimu kwa ukaribu na Mhudumu wa Afya ngazi ya Jamii