Header Ads Widget

AUAWA BAADA YA KUGOMA KUFANYA MAPENZI MWANZA

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mwanza, ACP Jumanne Muliro.

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Anastazia Zacharia, amefariki dunia baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani na mume wake, baada ya kumtaka wapime kwanza afya zao kabla ya kushiriki tendo la ndoa, kwani mume wake huyo hakuwepo nyumbani kwa muda wa mwezi mmoja.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP Jumanne Muliro na kusema kuwa tukio hilo limetokea Aprili 26,2020 majira ya saa 4:00 usiku, baada ya mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina la Laurent Herman kutakiwa na mke wake, apime afya na ndipo alipoamua kumpiga na kitu kizito kichwani na kupelekea kufariki dunia.

Kamanda Muliro ameongeza kuwa mara baada ya kufanya tukio hilo, mwanaume huyo aliamua kunywa sumu ya madawa ya kilimo kwa lengo la kujiua, ambapo jana Aprili 27, 2020, na yeye alipoteza maisha.

Katika tukio lingine Kamanda Muliro amesema, katika Mtaa wa Mtakuja wilayani Ilemela, wameokotwa watoto wawili mmoja akiwa na umri wa mwaka mmoja na mwingine akikadiriwa kuwa na miezi mitatu, wakiwa hai kwenye shamba la mpunga huku Jeshi hilo likiendelea kuwatafuta wazazi wa watoto hao ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
 CHANZO- EATV
TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp 0756472807