Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Teknolojia na Habari ya Nukta Africa , Nuzulack Dausen, amesema taarifa sahihi ni jambo nyeti katika jamii kwa kuwa zina nafasi kubwa katika kusaidia wananchi na taasisi kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya maendeleo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Nukta Africa, Nuzulack Dausen, akizungumza katika mafunzo hayo.
Dausen ameeleza kuwa kuenea kwa taarifa potofu na matamshi ya chuki (hate speech) kunaweza kuathiri sekta mbalimbali na kuhatarisha ustawi wa jamii, hivyo ni muhimu kwa waandishi wa habari kuwa na ujuzi na kutumia mbinu za kisasa katika kubaini, kuchambua na kukabiliana na taarifa potofu pamoja na maudhui ya chuki.
Ameongeza kuwa, mafunzo hayo yanatoa fursa kwa wadau wa habari kujengeana uwezo na kubadilishana uzoefu kuhusu mbinu za kisasa za kukabiliana na habari potofu katika vyombo vya habari, kwa lengo la kusaidia jamii kupata taarifa sahihi na kufanya maamuzi yenye tija kwa maendeleo yao.
Amesema Mafunzo hayo ni sehemu ya programu ya Maabara ya Fikra Bunifu na Uvumbuzi (Design Thinking and Innovation Lab) inayosimamiwa na IMS na washirika wake, ikiwa na lengo la kuwajengea washiriki uelewa na uwezo wa kutumia kanuni, hatua na mbinu za Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (Human-Centred Design - HCD katika kutambua na kutatua changamoto zinazohusiana na taarifa potofu.
Kwa upande wake, Programu Meneja wa Shirika la International Media Support (IMS), Fausta Musokwa, amesema taasisi hiyo inashirikiana na wadau wa habari nchini Tanzania kutekeleza mradi wa kukabiliana na taarifa zisizo sahihi na taarifa za upotoshaji (misinformation na disinformation), kwa kuvijengea uwezo vyombo vya habari kutumia mbinu sahihi za kuelimisha jamii.
Programu Meneja wa International Media Support (IMS), Fausta Musokwa.
Musokwa amesema ni muhimu kuongeza ubunifu katika vyombo vya habari na kuwajengea uwezo waandishi wa habari kukabiliana na taarifa potofu na matamshi ya chuki (hate speech), akisisitiza kuwa waandishi wana nafasi muhimu katika kulinda demokrasia kwa kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi na zilizothibitishwa.
“Ni muhimu kuongeza ubunifu katika vyombo vya habari kwa sababu mwandishi wa habari ni mlinzi wa demokrasia. Mwandishi wa habari ni askari muhimu anayewawezesha wananchi kupata taarifa sahihi na tunapaswa kujitofautisha na makundi mengine ya kijamii yanayoeneza taarifa mtandaoni, ‘citizen journalists’,” amesema.
Amefafanua kuwa kuenea kwa taarifa potofu na maudhui ya chuki ni changamoto inayoongezeka duniani, huku matumizi ya simu janja na upatikanaji mpana wa intaneti vikichochea kasi ya usambazaji wa taarifa hizo.
Amesema hali hiyo inaweza kuleta madhara kwa watu binafsi na jamii, ikiwemo kuathiri maamuzi ya wananchi, hivyo vyombo vya habari vinapaswa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi na za kuaminika.

Naye Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Dkt. Hellen Maziku, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwanzilishi wa HCD Services Tanzania, amesema mafunzo hayo yanasisitiza umuhimu wa kutumia mtazamo unaomlenga mtumiaji katika kutafuta suluhisho la changamoto ya taarifa potofu.
Amesema mtazamo huo unazingatia mahitaji, matarajio, uzoefu na tabia za wananchi wanaokumbwa na changamoto ya taarifa potofu, hatua inayolenga kuhakikisha suluhisho zinazobuniwa zinakidhi mahitaji halisi ya watumiaji wa taarifa.
Washiriki wa mafunzo hayo wamesema yatawasaidia kupata uelewa na mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kutambua, kuchambua na kukabiliana na habari potofu na taarifa za upotoshaji katika kazi zao za kila siku.
Wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuongeza umakini katika kuchakata taarifa kabla ya kuzifikisha kwa wananchi, hatua ambayo itachangia kuimarisha uaminifu wa jamii kwa vyombo vya habari na kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi na zenye manufaa kwa maisha yao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya teknolojia na habari ya Nukta Africa, Nuzulack Dausen, akizungumza wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu na matamshi ya chuki (hate speech).

Programu Meneja wa International Media Support (IMS), Fausta Musokwa, akizungumza wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu na matamshi ya chuki (hate speech).

Mwezeshaji wa mafunzo hayo kuhusu Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD), Dkt. Hellen Maziku, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwanzilishi wa HCD Services Tanzania, akizungumza wakati wa mafunzo hayo.

Mkurugenzi wa Malunde Media, Kadama Malunde, akichangia hoja wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu na matamshi ya chuki (hate speech).