` YOUNG WOMEN LEADERSHIP WATAMBULISHA MRADI WA MWANAMKE NI SEHEMU YA MAAMUZI SHIRIKI NAYE

WANDAMAN HOTEL

YOUNG WOMEN LEADERSHIP WATAMBULISHA MRADI WA MWANAMKE NI SEHEMU YA MAAMUZI SHIRIKI NAYE

 

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SHIRIKA la Young Women Leadership limetambulisha mradi wa Mwanamke ni sehemu ya maamuzi shiriki Naye, katika Kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga, ukiwa na lengo la kuwawezesha wanawake kushiriki katika vyombo vya maamuzi na ngazi ya familia.

TAZAMA VIDEO👇👇


Akizungumza leo Septemba 9, 2026, wakati wa utambulisho wa mradi huo, Meneja wa Miradi wa shirika hilo, Veronica Masawe, amesema mradi huo katika Manispaa ya Shinyanga unatekelezwa katika Kata mbili ya Kizumbi na Mwawaza.
Amesema, mradi huo unalengwa wanawake vijana kuanzia umri wa miaka 18 hadi 35 kwa lengo la kuwajengea uwezo ili waweze kujiimarisha kiuongozi, pamoja na kushiriki kwenye vyombo vya maamuzi na Nyanja za uongozi kuanzia ngazi ya familia hadi kwenye jamii.

“Tuwaombe wananchi wote tunapokuwa kwenye utekelezaji wa mradi huu, tushirikiane kwa pamoja kupaza sauti kwa ajili ya kuwaimarisha wanawake ili waweze kujengeka kujisimamia pamoja na kunufaika na fursa mbalimbali kwenye jamii, ikiwamo ya uongozi,” amesema Masawe.
Aidha, amesema mila na desturi kandamizi ni miongoni mwa changamoto ambazo zinazowakabili wanawake katika kushiriki katika vyombo vya maamuzi.

Amesema, mila hizo zimekuwa zikiwabana wanawake na kuwanyima haki zao mbalimbali, ikiwamo nafasi ya kutoa maoni na kushiriki katika maamuzi yanayohusu familia na jamii kwa ujumla.
“Mojawapo ya changamoto tunazokutana nazo katika jamii ni mila na desturi kandamizi ambazo zimekuwa zikiwabana wanawake na kuwanyima haki zao mbalimbali, hasa katika kushiriki kwenye vyombo vya maamuzi,” amesema Masawe.

Amesema kupitia mradi huo, shirika linatarajia kuwawezesha wanawake kutambua haki zao, kuongeza ushiriki wao katika vikao vya maamuzi na kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wa kikao hicho, akiwamo Cotholata Dominic, amesema mfumo dume bado ni changamoto katika jamii, hivyo mradi huo utasaidia kuwawezesha wanawake kuondokana na vikwazo vinavyowazuia kushiriki kikamilifu katika maamuzi.

Amesema wanawake wakipata uelewa na uwezo wa kiuchumi, watakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kushiriki katika maamuzi ndani ya familia na jamii.

Mradi huu umefadhiliwa na mfadhili Global Affairs Canada(GAC),mshirika mkuu anayesimamia utekelezaji Cuso International na Washirika wa kimkakati katika utekelezaji wa mradi ambao ni Msichana Initiatives,Women Fund Tanzania Trust na Tanzania Health Forum Initiative.


TAZAMA PICHA👇👇
Meneja miradi kutoka Shirika la Young Women Leadership Veronica Masawe akitambulisha mradi.
Meneja miradi kutoka Shirika la Young Women Leadership Veronica Masawe akitambulisha mradi.
Meneja miradi kutoka Shirika la Young Women Leadership Veronica Masawe akitambulisha mradi.
Meneja miradi kutoka Shirika la Young Women Leadership Veronica Masawe akitambulisha mradi.
Meneja miradi kutoka Shirika la Young Women Leadership Veronica Masawe akitambulisha mradi.
Diwani wa Mwawaza Edwin Mwasha akizungumza kwenye kikao hicho.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464