` WAANDISHI WA HABARI MKOANI SHINYANGA WAMEPATIWA MAFUNZO NA TPDC

WANDAMAN HOTEL

WAANDISHI WA HABARI MKOANI SHINYANGA WAMEPATIWA MAFUNZO NA TPDC

 

WAANDISHI WA HABARI MKOANI SHINYANGA WAMEPATIWA MAFUNZO NA TPDC

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga, wamepewa mafunzo na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Mafunzo hayo yamefanyika leo Septemba 4,2026 Mjini Shinyanga.

Mgeni Rasmi Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga David Lyamongi, akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo ya siku moja, amesema waandishi wa habari wanapaswa kueleza ubora na manufaa ya mradi huo wa bomba la mafuta ghafi, na faida zake, pamoja na kuhamasisha wananchi kulinda miundombinu yake.
“Tunajua waandishi ni nguzo ya nne ya dola, hivyo nyie mkiongea vizuri, wananchi wataelewa na kulinda miundombinu ya mradi wa bomba la mafuta,” amesema Lyamongi.

Mkuu wa kitengo cha uhusiano na Mawasiliano kutoka TPDC, Marie Msellemu, amesema warsha hiyo ni mkakati wa shirika kuwa karibu na wadau wake, na kuwaelezea kuhusu miradi ya gesi asilia na bomba la mafuta ghafi, na kwamba Januari 2027 wanaweza kupata tone la kwanza la mafuta ya Petroli.
Amesema, wameandaa warsha hiyo kwa waandishi wa habari, ili waweze kutumia kalamu zao kuwaeleza wananchi kuhusu mambo ambayo TPDC inafanya, pamoja na namna watakavyonufaika na mradi huo wa bomba la mafuta ghafi la afrika mashariki.


Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru, ameishukuru TPDC kwa mafunzo hayo, akisema yamewaongezea waandishi wa habari ujuzi wa kuandika kwa ufasaha kuhusu masuala ya mafuta na gesi asilia.

TAZAMA PICHA👇👇
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga David Lyamongi akizungumza.
Mkuu wa kitengo cha Uhusiano nma Mawasiliano TPDC Marie Msellemu.
Kaimu Mratibu wa Bomba la Mafuta Ghafi Afrika Mashariki TPDC Jumanne Said.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Shinyanga SPC Greyson Kakuru akizungumza.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464