` WAZIRI SANGU ASISITIZA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI, DKT. NCHEMBA ACHANGIA MILIONI 25 AICT

WANDAMAN HOTEL

WAZIRI SANGU ASISITIZA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI, DKT. NCHEMBA ACHANGIA MILIONI 25 AICT

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Clement Sangu, amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na taasisi za dini katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa, huku akitoa wito kwa viongozi wa kiroho kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha amani, mshikamano, na maadili mema ndani ya jamii.

Akizungumza mkoani Geita wakati akimwakilisha Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba katika maadhimisho ya miaka 25 ya Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) na Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la Nyanza, Mhe. Sangu alieleza kuwa jubilei hiyo ni ushuhuda thabiti wa uaminifu, uvumilivu, na kujitoa kwa viongozi na waumini katika kulitumikia kanisa hilo kwa kipindi chote cha robo karne.

Katika hafla hiyo iliyofanyika tarehe 23 Agosti 2026, Mhe. Sangu alitumia fursa hiyo kumkabidhi Mchungaji Kiongozi wa AICT Pastoreti ya Nyanza, Mchungaji Emmanuel Lwangaka, mchango wa Shilingi milioni 25 uliotolewa na Waziri Mkuu Dkt. Nchemba kwa ajili ya kusaidia ukamilishaji wa ujenzi wa jengo jipya la kanisa hilo ambalo linakadiriwa kugharimu kiasi cha Shilingi milioni 600 ;na litakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia waumini 700 kwa wakati mmoja, huku akitoa wito kwa waumini

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Clement Sangu, amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na taasisi za dini katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa, huku akitoa wito kwa viongozi wa kiroho kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha amani, mshikamano, na maadili mema ndani ya jamii.

Akizungumza mkoani Geita wakati akimwakilisha Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba katika maadhimisho ya miaka 25 ya Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) na Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la Nyanza, Mhe. Sangu alieleza kuwa jubilei hiyo ni ushuhuda thabiti wa uaminifu, uvumilivu, na kujitoa kwa viongozi na waumini katika kulitumikia kanisa hilo kwa kipindi chote cha robo karne.

Katika hafla hiyo iliyofanyika tarehe 23 Agosti 2026, Mhe. Sangu alitumia fursa hiyo kumkabidhi Mchungaji Kiongozi wa AICT Pastoreti ya Nyanza, Mchungaji Emmanuel Lwangaka, mchango wa Shilingi milioni 25 uliotolewa na Waziri Mkuu Dkt. Nchemba kwa ajili ya kusaidia ukamilishaji wa ujenzi wa jengo jipya la kanisa hilo ambalo linakadiriwa kugharimu kiasi cha Shilingi milioni 600 ;na litakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia waumini 700 kwa wakati mmoja, huku akitoa wito kwa waumini na wafanyabiashara kuendelea kuchangia mradi huo.

Aidha katika harambee hiyo waziri Sangu alichangia shilingi milioni 
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kushirikiana na makundi yote ya kijamii na viongozi wa dini ili kuleta tija katika ustawi na maendeleo ya wananchi.

Naye Katibu Mkuu wa AICT, Kaseha Wilson Mengi, alitoa shukrani za dhati kwa viongozi hao wa serikali kwa kukubali kuungana na waumini katika sherehe hizo kubwa zilizohudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Geita, Bi. Lucy Beda, pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka ndani na nje ya mkoa huo.

Ibada hiyo imeongozwa na Mchungaji Kiongozi wa AICT Pastoreti ya Nyanza, Mchungaji Emmanuel Lwangaka na kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali wakiongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Geita Bi. Lucy Beda, Viongozi wa Kanisa la AICT na makanisa mengine, pamoja na Waumini na Wadau.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464