
Na Neema Sawaka,Kahama
Waathirika na waraibu wa dawa za kulevya wanaopatiwa matibabu katika kituo cha Tiba na huduma kwa waraibu kilichopo katika hospital ya manispaa ya kahama mkoani Shinyanga wamemshukuru kamishna Jenerali wamamlaka ya kudhibiti kupambana na madawa ya kulevya Aretas James Lyimo kwa juhudi zinazoendelea za kudhibiti biashara ya usambazaji na uuzwaji wa dawa zakulevya nchini.
Wamesema hatuazinazochukuliwa na serikali dhidi ya wauzaji na wasambazaji wa dawa hizo zimekuwa na mchango mkubwa katika kupunguza na kukomesha upatikanaji wa madawa ya kulevya ,na kuwapa fursa waathirika kupata matibabu na kurejea katika maisha ya kawaida.
Hayo yamebainika wakati mwenge wa uhuru ulipozindua jengo la kituo cha Tiba na huduma kwa waraibu wa dawa za kulevya kilichopo hospital ya manispaa ya Kahama ,lililojegwa kwa lengo la kutoa huduma za matibabu na
urekebishwaji wa afya kwa waathirika wa dawa za kulevya.
Jengo hilo ambalo limegharimu shilingi milioni 467,fedha zilizotolewa na serikali kupitia mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya ,kwa len go la kuimarisha huduma kwa watu walioathirika na matumizi ya dawa hizo,
Aidha kituo hicho kinasaidia waathirika kupata matibabu na huduma mbalimbali zinazolenga kurejesha afya zao ,kwakuwawezesha kuacha matumizi ya dawa za kulevya nahatimaye kurejea katika shughuri za kawaida za kijamii na kiuchumi.
Kwa upande wake Muuguzi kiongozi wa kituo hicho Grace Nzagamba amesema kituo hicho kwa sasa kinahudumia kati ya waraibu 30 _48 ,huku mwitikio wa wananchi wanaohitaji huduma kuendelea kuwa mkubwa .
Amesema baadhi ya waliowahi kupata matibabu katika kituo hicho ,wamefanikiwa kuacha matumizi ya dawa za kulevya na kurejea katika maisha ya kawaida huku wengine matibabu na. ufuatiliaji.
"Baadhi ya waliomaliza matibabu wamepona na sasawanaendelea na shughuli Mbali mbali za kujenga Taifa alisema Grace Nzagamba
Kwa upande wake,mmoja wa waathirika hao Multaz Maganga,amesema Alianza kutumia dawa za kulevya mwaka 2005, lakini kwa sasa kaacha matumizi hayo
Amesema hali ya upatikanaji wa dawa za kulevya kwa sasa si kama ilivyokuwa miaka 3 ya nyuma na kueleza kuwa hatua za kudhibiti zimechangia kupunguza upatikanaji wake.


Multaz amesema juhudi za serikali kupitia kamishina lyimo imekuwa mhimu katika kuwasaidia waathirika kupata nafasi ya kuacha matumizi na kuanza maisha mapya.
Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa, Wazo Mwang'onda,amepongeza ujenzi wa kituo hicho na juhudi zilizofanywa katika kutoa matibabu kwa waraibu wa dawa za kulevya.
Amesema ni mhimu kwa waraibu wanaopona na kurejea kwenye hali zao za kawaida kupewa fursa za kiuchumi ili waweze kujitegemea na kuendelea kushiriki katika shughuli za maendeleo ya Taifa.
Ameeleza kuwa waraibu wanapaswa kuwekewa programu mbalimbali za kuwawezesha kiuchumi ikiwepo mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa makundi ya vijana wanawake na watu wenye ulemavu ili waweze kuanzisha shughuri za uzalishaji.
Aliongeza kuwa uwepo wa kituo hicho umeonekana kuwa hatua muhimu katika kuunganisha juhudi za kuzuia dawa za kulevya,kwa kutoa matibabu kwa waathirika na kuwawezesha waliopona kurejea katika maisha yenye tija,huku wana nchi wakihimizwa kuendelea kushirikiana na serikali kwa kutoa taarifa kuhusu biashara za usambazaji wa dawa hizo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464