Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya CRDB, Xavery Makwi, akiimba shairi wakati wa uzinduzi wa Tawi la Benki ya CRDB Tinde mkoani Shinyanga.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Michael Mwang’onda, akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakifurahia wakati wa uzinduzi wa Tawi la Benki ya CRDB Tinde mkoani Shinyanga.
Na Stella Herman,Shinyanga
Upatikanaji wa huduma za kifedha umeendelea kuimarika katika maeneo ya vijijini baada ya Benki ya CRDB kufungua tawi jipya katika eneo la Tinde mkoani Shinyanga, hatua inayolenga kuwafikishia wananchi huduma za kibenki kwa urahisi zaidi.
Tawi hilo lililopo Njiapanda ya Tinde, Kitongoji cha Uswahili, Kijiji cha Jomu, Wilaya ya Shinyanga, takribani kilomita 35 kutoka Shinyanga Mjini, limezinduliwa rasmi leo Alhamisi, Agosti 20, 2026, na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Michael Mwang’onda.
Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Mwang’onda ameipongeza CRDB kwa kuendelea kupanua wigo wa huduma zake na kuwekeza katika miundombinu ya kifedha inayowafikia wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.
“Nipende kuipongeza Benki ya CRDB kwa kuendelea kupanua wigo wa huduma zake na kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali nchini. Leo tupo hapa kushuhudia uzinduzi wa tawi jingine la benki hii katika eneo la Tinde, hatua inayoonesha namna benki hii inavyotambua mahitaji ya wananchi na kuyafanyia kazi,” amesema Mwang’onda.
Amesema CRDB imeendelea kuwa mshirika muhimu wa Serikali katika utekelezaji wa programu mbalimbali za kuwawezesha wananchi kiuchumi, akitolea mfano fedha zinazotolewa kwa makundi maalumu ambazo hupitia katika benki hiyo.
“Kati ya benki ambazo zinafanya kazi vyema na Serikali ni Benki ya CRDB. Fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya makundi maalumu kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi zinapita katika benki hii,” amesema.
Mwang’onda pia amepongeza CRDB kwa kushiriki katika programu na shughuli mbalimbali zinazolenga kuwawezesha vijana kiuchumi, ikiwemo utoaji wa mikopo.
“Pamoja na mikopo inayotolewa kwa ajili ya kuwawezesha vijana kiuchumi, zaidi ya milioni 200, CRDB inahusika pia. Hii inaonesha umahiri wa utendaji kazi katika benki yenu, hivyo niwapongeze sana,” amesema.
Ameitaka CRDB kuendelea kupanua huduma zake katika maeneo mengine na kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanapata fursa ya kutumia huduma za kifedha, hatua ambayo amesema itasaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
“Na niendelee tu kuwapongeza na zaidi ya yote, nawasihi kuendelea kuwahudumia wananchi wenu ili kuhakikisha kila Mtanzania anainuka kiuchumi,” amesema Mwang’onda.

Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Tawi la Benki ya CRDB Tinde mkoani Shinyanga wakati wa uzinduzi rasmi wa tawi hilo.
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Tawi la Benki ya CRDB Tinde mkoani Shinyanga wakati wa uzinduzi rasmi wa tawi hilo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Michael Mwang’onda, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi la Benki ya CRDB Tinde mkoani Shinyanga.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Michael Mwang’onda, akitembelea Tawi la Benki ya CRDB Tinde mkoani Shinyanga wakati wa uzinduzi rasmi wa tawi hilo.
Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya CRDB, Xavery Makwi, akiimba shairi wakati wa uzinduzi wa Tawi la Benki ya CRDB Tinde mkoani Shinyanga.

Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru wakati wa uzinduzi wa Tawi la Benki ya CRDB Tinde mkoani Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru wakati wa uzinduzi wa Tawi la Benki ya CRDB Tinde mkoani Shinyanga.
Mwenge wa Uhuru ukiondoka katika Tawi la Benki ya CRDB Tinde mkoani Shinyanga baada ya kukamilika kwa shughuli za uzinduzi wa tawi hilo.
Mwenge wa Uhuru ukiondoka katika Tawi la Benki ya CRDB Tinde mkoani Shinyanga baada ya kukamilika kwa shughuli za uzinduzi wa tawi hilo.
Wafanyakazi wa Tawi la Benki ya CRDB Tinde mkoani Shinyanga.
kelezaji wa programu mbalimbali zinazolenga kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mikopo wa CRDB, Xavery Makwi, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dkt. Abdulmajid Mussa Nsekela, amewataka wananchi wa Tinde na maeneo jirani kutumia fursa za mikopo na huduma za kifedha zinazotolewa na benki hiyo.
Amesema CRDB imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi trilioni 31 kwa makundi mbalimbali, yakiwemo wakulima, wafanyabiashara, watumishi, wastaafu na watu binafsi, huku akisisitiza kuwa uwepo wa tawi hilo utawawezesha wananchi kupata huduma bila kusafiri hadi Shinyanga Mjini.
Makwi amesema Tawi la Tinde ni miongoni mwa matawi 25 ya CRDB katika Kanda ya Magharibi, inayojumuisha Shinyanga, Tabora, Kigoma na Geita.
Ameongeza kuwa ujenzi wa tawi hilo umegharimu shilingi milioni 650, zilizotumika katika ununuzi wa ardhi, ujenzi wa jengo na uwekaji wa vifaa, huku tawi hilo likihamia katika jengo jipya Aprili 2026.
Kwa upande wao, wananchi wa Tinde wameishukuru Benki ya CRDB kwa kuwasogezea huduma za kifedha karibu na maeneo yao, wakisema uwepo wa tawi hilo utawarahisishia kupata huduma za kibenki bila kulazimika kusafiri hadi Shinyanga Mjini.
Wamesema awali walilazimika kutumia muda na gharama za usafiri kwenda Shinyanga mjini kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za kibenki, ikiwemo kuweka na kutoa fedha, lakini uwepo wa tawi hilo Tinde umewaondolea changamoto hiyo.
Wamesema hatua hiyo pia itaongeza urahisi na usalama katika matumizi ya huduma za kifedha, huku wakiitaja kuwa fursa muhimu kwa wakazi wa Tinde na maeneo jirani katika kukuza shughuli zao za kiuchumi.



















































































