` WAGENI WAMIMINIKA BANDA LA MALIASILI MAONESHO YA NANE NANE

WANDAMAN HOTEL

WAGENI WAMIMINIKA BANDA LA MALIASILI MAONESHO YA NANE NANE

 

📌 Wamo Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala 

📌 Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wapatiwa elimu ya uhifadhi, malikale, wanyamapori, misitu na nyuki

📌 'Kasongoyeye' apata umaarufu mkubwa Banda la Maliasili

Na Neema Chalila Mbuja, Dodoma

WAGENI mbalimbali wameendelea kumiminika kwenye Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya Siku ya Wakulima Duniani (NANE NANE), kujionea shughuli mbalimbali za uhifadhi na wanyamapori zinazofanywa na Wizara.

Miongoni mwa wageni waliotembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii ni pamoja na Wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala mbalimbali ambapo waliipongeza Wizara kwa ushiriki wa Maonesho hayo ya NANE NANE kwani wamekuwa wakichagiza uwepo wa wananchi wengi wanaokuja kufanya utalii wa ndani wa kuona wanyamapori.

Makatibu Tawala hao ni pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kongwa Sozi Ngate, Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma Mjini Sakina Mbugi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kondoa Christina Kalekezi na Wakuu  wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri na Mpwapwa Dkt. Sophia Kizigo.

Viongozi hao wamesema kila mwaka Wizara ya Maliasili na Utalii imekuwa ikipokea wageni wengi hususani wananchi na wanafunzi wanaotembelea banda lake kujifunza elimu kuhusu uhifadhi, wanyamapori, malikale, misitu na nyuki.

Katika hatua nyingine Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii Imepokea wananfunzi zaidi ya elfu moja waliofika kwa ajili ya kupata wa elimu na kuona wanyamapori hai ambapo wengi wao wamevutiwa na mnyama  Ngiri maarufu kama Kasongoyeye ambaye  ana umaarufu mkubwa kutokana na tabia yake na kutokuwa na uoga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464