` MWIGIZAJI LUCY KOMBA AOMBA MSAMAHA KWA SERIKALI NA WANANCHI KUPITIA UKURASA WAKE WA INSTAGRAM

WANDAMAN HOTEL

MWIGIZAJI LUCY KOMBA AOMBA MSAMAHA KWA SERIKALI NA WANANCHI KUPITIA UKURASA WAKE WA INSTAGRAM

Mwigizaji nguli wa filamu za Kitanzania anayeishi nchini Denmark, Lucy Komba, ameomba msamaha rasmi kwa Serikali na wananchi wote wa Tanzania kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Instagram, kufuatia vitendo vyake vya awali vya kuhamasisha na kuchochea maandamano wakati wa ghasia nchini, hatua iliyokuja baada ya awali kujaribu kukana kuhusika kwake kabla ya video zinazomwonesha kufichuliwa na kusambaa mtandaoni.
Msanii huyo, ambaye alianza safari yake ya sanaa kupitia kundi la Kaole na kushiriki kwenye filamu mbalimbali zilizotamba kabla ya kuhamishia makazi yake nchini Denmark, alitumia ukurasa wake huo wa Instagram kukiri makosa na kueleza wazi kuwa kilichotokea kipindi cha nyuma kimewakwaza Watanzania wengi, huku akisisitiza kuwa yeye kama mtanzania anaipenda sana nchi yake na anathamini amani iliyopo.

Kitendo hiki cha kuomba radhi kupitia mtandao huo kimefuatia shinikizo kubwa kutoka kwa jamii na kauli za kukumbushia makosa yake ya nyuma zilizotolewa na wadau mbalimbali akiwemo anayefahamika kama Kaka wa Taifa, ambaye alimweka wazi kupitia video zilizofichua ukweli wa mambo aliyoyafanya hapo awali baada ya msanii huyo awali kujaribu kuyakanusha, jambo lililomlazimu kujitokeza hadharani kupitia ukurasa wake huo wa Instagram ili kuomba msamaha na kutafuta maridhiano na wananchi pamoja na mamlaka za nchi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464