` MKURUGENZI WA SHULE ZA ANDERLEK NA ROCKEN HILL ATUMA UJUMBE MZITO KWA VIJANA AWAPA MBINU ZA MAFANIKIO

WANDAMAN HOTEL

MKURUGENZI WA SHULE ZA ANDERLEK NA ROCKEN HILL ATUMA UJUMBE MZITO KWA VIJANA AWAPA MBINU ZA MAFANIKIO


MKURUGENZI wa Shule za Anderlek Ridges na Rocken Hill, Sir Alexander Kazimili


Na Neema Sawaka, Kahama

Shule za Anderlek Ridges na Rocken Hill,zimefanya mahafali ya 22 huku Mkurugenzi wa shule hizo Sir Alexander Kazimili akatumia fursa hiyo kusisitiza maadili kwa vijana kutokana na  mmomonyoko wa maadili katika jamii.
Kazimili amesema  baadhi ya vijana wamekuwa wakiwatishia hata wazazi wao na kufikia hatua ya kutaka kurithi mali badala ya kujenga maisha yao kupitia bidii,ambapo amewaasa wahitimu kutumia elimu waliyoipata kuwa mabalozi wa maadili Mama kutokana na shule hiyo kuwajenga katika msingi wa maadili mema.

Katika hatua nyingine Sir Alexander Kazimili amewataka vijana  kutumia akili, ubunifu na maarifa kama fursa ya kujiajiri na kuongeza kipato na kusisitiza kuwa mafanikio katika maisha yanahitaji maono, bidii na ubunifu.

Kazimili ameyasema hayo wakati wa mahafali ya 22 ya Shule ya Sekondari Anderlek Ridges na Shule ya Msingi Rocken Hill, zilizopo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, ambapo amewataka vijana kuendana na dunia ya utandawazi inayotawaliwa na ubunifu, teknolojia na ushindani.

Amesema vijana wanapaswa kujenga uwezo wa kushindana ndani na nje ya nchi kwa kuwa dunia ya sasa inahitaji watu wenye maarifa, uwezo wa kujitambua, bidii na ndoto za maisha.

“Mimi nilianza ujasiriamali na kufundisha nikiwa bado shuleni na ndiyo ilikuwa ndoto yangu, na leo imetimia. Unatakiwa maono yako uyaanze chini na kwenda juu. Lakini wengine huanzia juu kwenda chini. Mambo ya akili unde yatumike kama fursa, lakini imekuwa tofauti, vijana wanatumia kwenda kinyume na maadili,” amesema Kazimili.

Kwa upande wake, mgeni rasmi katika mahafali hayo, Daktari wa Magonjwa ya Moyo nchini Urusi na mhadhiri wa Chuo Kikuu, Dkt. Joseph Charles, ambaye ni mmoja wa wahitimu wa shule hiyo, amesema historia ya taasisi hiyo ni ushahidi kuwa maono, ujasiri na bidii vinaweza kuleta mafanikio.

Dkt. Charles amesema shule hiyo ilianzishwa mwaka 1999 ikiwa na jengo moja lenye vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja, lakini imeendelea kukua na kufikia hatua ya kutambulika na kuwa taasisi yenye maendeleo makubwa.

“Tunaona hii leo ni mtu mmoja alikuwa na maono na ujasiri mkubwa sana. Haikuwa rahisi, mara nyingi binadamu huanzia chini na mwanzo unakuwa mgumu, huku akikumbana na vikwazo,” amesema Dkt. Charles.

Amesema mtu anapoamini katika jambo, akaliweka kwenye maono na kulifanyia kazi kwa bidii, anaweza kufikia ndoto zake, huku akimpongeza Mkurugenzi Kazimili kwa kutokata tamaa hadi kutimiza ndoto yake.

Dkt. Charles pia amewataka wanafunzi kutambua kuwa elimu wanayoipata shuleni haipaswi kuishia kwenye kufaulu mitihani, bali inapaswa kuwajengea maarifa na uwezo wa kukabiliana na maisha na kulitumikia taifa.

Amesema safari yake ya mafanikio ilianzia katika Shule ya Msingi Rocken Hill na baadaye kufika nchini Urusi ambako amekuwa akifanya kazi kama daktari wa magonjwa ya moyo.

“Wanafunzi wanapaswa kuendelea kuwasikiliza walimu na kuwa na bidii ili waweze kutimiza ndoto zao. Eneo la shule si kufaulu mitihani peke

\















Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464