
SIKU moja baada ya Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kutangaza kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais wa Tanzania na Rais samia Suluhu Hassan kuridhia barua yake, Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imemvua uanachama.
Uamuzi huo umefanywa na Halmashauri Kuu ya CCM katika kikao chake kilichofanyika leo, Agosti 26, 2026 chini ya Mwenyekiti wake Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza na waandishi wa habari leo usiku Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Asha Rose Migiro amesema “Kamati Kuu imejadili kuhusu suala la nidhamu na maadili ambalo lilikuwa linamkabili Emmanuel Nchimbi, na baada ya kuzingatia taarifa zote zilizokuwepo ilithibitika kwamba katiba ya CCM na kanuni zake zilikiukwa, na hivyo Nchimbi amefukuzwa uanachama.”
Dkt. Nchimbi alitangaza kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais na kustaafu shughuli za kisiasa jana, Agosti 25, 2026.
Katika hatua nyingine, Halmashauri Kuu ya CCM imetoa tamko la kumpendekeza rasmi jina la Mbunge wa Jimbo la Chamwino na Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, kuchukua nafasi ya Makamu wa Rais.
Pendekezo hilo limefikiwa katika kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa mujibu wa utaratibu, baada ya CCM kupendekeza jina hilo, jina la Deogratius Ndejembi litawasilishwa Bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura na Wabunge.
Ndejembi ataweza kushika rasmi nafasi ya Makamu wa Rais endapo atapata kura zinazohitajika kutoka kwa Wabunge, kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.