Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wamejadili taarifa ya hesabu za mwisho za halmashauri kuishia juni 2026, huku makampuni yanayodaiwa na halmashauri fedha za ushuru wa huduma kuchukuliwa hatua.
Mkutano huo wa Baraza hilo Maalumu umefanyika leo Agosti 31,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Ibrahimu Makana akizungumza kwenye Baraza hilo wakati akitoa salamu za Mkoa, amesema makampuni yote ambayo yanadaiwa na halmashauri hiyo yawasilishwe taarifa zao kwenye Ofisi ya Mkoa ili wachukue hatua.
Amesema, hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), linalotaka makampuni hayo kuwajibika kulipa ushuru huo.
Amemwagiza pia Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, kuandaa mkakati wa kulipa madeni ambayo halmashauri inadaiwa na wazabuni, pamoja na kuhakikisha halmashauri haizalishi madeni mapya.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Seth Msangwa, amesema kwa upande wa madeni ambayo halmashauri inadaiwa na watumishi ni muhimu kuanza kuwalipa madeni hayo kwa kuanza na wastaafu.
Kwa upande wake Mweka Hazina wa halmashauri hiyo, CPA Shimi Emmanuel, amesema halmashauri hiyo imeanza kupunguza madeni inayodaiwa, kutoka bilioni 1.9 hadi bilioni 1.7.
TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Seth Msangwa akizungumza.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk. Kalekwa Kasanga akizungumza.
Mwekahazina wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga CPA Shimi Emmanuel akiwassilisha taarifa.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Ibrahimu Makana akizungumza.
Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Said Kitinga akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela akizungumza.