Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Wanafunzi wa shule ya Msingi na awali Hinaya iliyopo Kata ya Isikiya wilaya ya Uyui mkoani Tabora, wamefanya utalii wa ndani kwa kutembelea Jambo Zoo mkoani Shinyanga, ili kujifunza kuhusu wanyama, maisha yao na aina ya vyakula wanavyokula.
TAZAMA VIDEO 👇👇
Wamefanya utalii huo leo, Agosti 27, 2026, wakiwa wameambatana na walimu wao.
Mmoja wa wanafunzi hao Brayan Tomy, amesema wamepata fursa ya kuwaona wanyama mbalimbali, na kwamba ziara hiyo imewasaidia kujifunza mambo mengi kuhusu maisha ya wanyama.
“Tumewaona wanyama wengi, na tumejifunza mambo mbalimbali kuhusu maisha yao na vyakula wanavyokula,” amesema Tomy.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Adamini Kijaji, amesema wameamua kufanya utalii huo wa ndani, ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo kwa kuwaona wanyama moja kwa moja.
Amesema, kujifunza kwa vitendo, kunawasaidia wanafunzi kuelewa vizuri zaidi masomo wanayofundishwa darasani.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464