` AZZA AHITIMISHA ZIARA KIJIJI KWA KIJIJI ITWANGI, ATOA PONGEZI KWA RAIS SAMIA KWA MIRADI YA MAENDELEO

WANDAMAN HOTEL

AZZA AHITIMISHA ZIARA KIJIJI KWA KIJIJI ITWANGI, ATOA PONGEZI KWA RAIS SAMIA KWA MIRADI YA MAENDELEO

 

 Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ihalo  kata ya Ilola wakati wa ziara yake ya kijiji kwa kijiji katika jimbo hilo, Agosti 16, 2026.

VIDEO👇👇


Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ihalo  kata ya Ilola wakati wa ziara yake ya kijiji kwa kijiji katika jimbo hilo, Agosti 16, 2026.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyanshimbi , Kata ya Puni, wakati wa ziara yake ya kijiji kwa kijiji katika Jimbo la Itwangi, Agosti 16, 2026.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyanshimbi, Kata ya Puni, wakati wa ziara yake ya kijiji kwa kijiji katika Jimbo la Itwangi, Agosti 16, 2026. Picha na Kadama Malunde


Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, amehitimisha ziara ya kijiji kwa kijiji katika jimbo hilo kwa awamu ya kwanza, huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
TAZAMA VIDEO👇👇



Azza amehitimisha ziara hiyo leo, Agosti 16, 2026, katika vijiji vya Ihalo na Nyanshimbi, ambapo amekutana na wananchi, kusikiliza kero zao na kuzitafutia majibu. Katika ziara hiyo, ameahidi kutoa mzani wa kupimia watoto kwa ajili ya huduma ya Kliniki ya Watoto katika Zahanati ya Nyanshimbi.

Mikutano hiyo ilihudhuriwa na wananchi kwa wingi, ambao walipata fursa ya kuwasilisha kero na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao, zikiwemo za miundombinu ya barabara, elimu, afya, maji na umeme.

Akizungumza na wananchi wakati wa ziara hiyo, Azza amesema ndani ya miezi minane tangu Rais Samia Suluhu Hassan aapishwe, Jimbo la Itwangi limepiga hatua katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara na madaraja yaliyokuwa yakileta changamoto kwa wananchi.

Amesema baadhi ya barabara na madaraja ambayo hapo awali yalikuwa korofi yameanza kufanyiwa kazi, huku utekelezaji wa miradi hiyo ukiendelea katika maeneo mengine ya jimbo hilo.

Kwa upande wa umeme, Azza amesema Jimbo la Itwangi limepata vitongoji 58 ambavyo vimeingizwa katika mpango wa kuunganishwa na huduma hiyo, huku nguzo zikiwa tayari zimefikishwa katika baadhi ya maeneo husika.

Aidha, amesema katika sekta ya afya, baadhi ya maboma ya zahanati yamekamilishwa na kuanza kutoa huduma kwa wananchi, huku mengine yakiwa yamefikia hatua ya kupauliwa.

“Kazi ya Mbunge ni kuwasemea wananchi wake na kutatuliwa kero zao. Niliwasemea na Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni sikivu na kero nyingi zimetekelezwa. Pamoja na mimi kuwa Mbunge wenu, nimemuunga mkono Rais wetu, na nilitoa fedha zangu na kupaua baadhi ya zahanati,” amesema Azza.

Akiwa katika Kijiji cha Nyanshimbi, Kata ya Puni, Azza amepokea kero ya ukosefu wa mzani wa kupimia watoto katika Kliniki ya Watoto ya Zahanati ya Nyanshimbi na kuahidi kuununua ili kuwezesha huduma hiyo kuendelea kutolewa kwa ufanisi.

Ziara hiyo ya kijiji kwa kijiji ya awamu ya kwanza imefanyika katika vijiji vya Butini, Nduguti, Ilobashi, Ng’wanhalanga, Usanda, Mwamanyuda, Didia, Nshinshinulu, Mwamkanga, Masunula, Mwamala, Ihalo na Nyanshimbi.

Ziara hiyo imelenga kuwafikia wananchi moja kwa moja, kusikiliza changamoto zao, kutoa majibu na kufuatilia utekelezaji wa mahitaji mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo la Itwangi.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464