` BANDORA AWATIA MOYO WANANCHI WA INALA, ACHANGIA MIFUKO MITANO YA SARUJI UJENZI WA OFISI YA KIJIJI

WANDAMAN HOTEL

BANDORA AWATIA MOYO WANANCHI WA INALA, ACHANGIA MIFUKO MITANO YA SARUJI UJENZI WA OFISI YA KIJIJI

 


Tabora

Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji, Ujenzi na Mazingira, Salum Bandora, amewatia moyo wananchi wa Inala, Kata ya Ndevelwa, kwa kupongeza juhudi zao katika ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Inala.

Bandora amewapongeza wananchi hao kwa kazi kubwa waliyoifanya pamoja na jitihada wanazoendelea nazo katika kuhakikisha ujenzi wa ofisi hiyo unakamilika. Katika kuunga mkono juhudi hizo, amechangia mifuko mitano ya saruji.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Bandora amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na kuwa na moyo wa kujitolea katika kutekeleza miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha huduma katika maeneo yao.

Kamati hiyo pia ilikagua ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto Manoleo pamoja na Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Misha, ikiwa ni sehemu ya kufuatilia maendeleo ya miradi ya ujenzi na kuhakikisha inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa.

“Nawatia moyo wananchi wa Inala, Kata ya Ndevelwa, kwa kazi kubwa mliyoifanya na mnayoendelea kuifanya. Nimeamua kuchangia mifuko mitano ya saruji ili kuunga mkono juhudi zenu.”amesema Bandora










Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464