` TAZAMA VIDEO-MBUNGE WA JIMBO LA KISHAPU LUCY MAYENGA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MAKABIDHIANO YA MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA GIMAGI- MAGALATA

WANDAMAN HOTEL

TAZAMA VIDEO-MBUNGE WA JIMBO LA KISHAPU LUCY MAYENGA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MAKABIDHIANO YA MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA GIMAGI- MAGALATA

TAZAMA VIDEO-MBUNGE WA JIMBO LA KISHAPU LUCY MAYENGA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MAKABIDHIANO UJENZI WA BARABARA YA GIMAGI- MAGALATA

Na Marco Maduhu, KISHAPU

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Lucy Mayenga, ameshuhudia utiaji saini makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Gimagi- Magalata ya kiwango cha changarawe baina ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini TARURA na Mkandarasi.

TAZAMA VIDEO👇👇


Makabidhiano hayo yamefanyika leo Julai 15,2027 katika Kijiji cha Magalata Kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu na kushuhudiwa pia na wananchi, ambao walimpongeza Mbunge huyo kwa kasi kubwa ya maendeleo ambayo anakuja nayo na kutatua kero zao.

Awali Kaimu Meneja wa TARURA wilayani Kishapu Mhandisi Hussein Shaweji, akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo, amesema urefu wake ni kilomita 35 lakini kwa awamu ya kwanza watajenga kilomita 20, na utekelezaji unaanza leo Julai 15. 2027 na utakwenda hadi Novemba 11.2026 na gharama zake ni milioni 699.3.
Amesema, katika ujenzi huo wa barabara pia utahusisha kujengwa daraja moja la mwandoma, na Makalavati 10, na kwamba mradi huo utakuwa na manufaa kwa wananchi, na kumaliza kero ya ubovu wa miundombinu ya barabara katika maeneo hayo.

“Leo tunaanza na ujenzi wa barabara kilomita 20, na awamu ya pili kilomita 15, tutaanza mwanzoni mwa Septemba ili kukamilisha kilomita zote 35,” amesema Mhandisi Shaweji.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kishapu Lucy Mayenga, amesema ujenzi wa barabara hiyo ni ahadi yake ambayo aliitoa kwa wananchi hao, na sasa amekuja kutimiza ahadi yake na kuijenga ili kuondoa kero hiyo.
Amesema, kutokana na ubovu wa barabara hiyo ilibidi apite katika kona zake k kwa kutafuta pesa, sababu barabara hiyo haikuwepo kwenye mpango wa bajeti, lakini amepambana ndipo pesa zikapatikana, na sasa inajengwa kwa kiwango cha changarawe.

“Pesa hizi hazikuwepo, lakini zimetoka nje ya bajeti, hivyo lazima tumshukuru Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ruhusa ya pesa kutumika hata kama baadhi ya maeneo pesa hazikutengwa na sasa wananchi wanakwensda kuondokana na kero ya ubovu wa barabara,” amesema Mayenga.

Naye Diwani wa Mwamalasa Bushi Mpina, amempongeza Mbunge huyo kwa kutatua kero hiyo ya ubovu wa barabara ambayo imekuwa changamoto kubwa kwa wananchi na hata kuathiri shughuli za kiuchumi na kijamii.
Kwa upande wake Mkandarasi Asha Said Amdani, amesema mradi huo watautekeleza kwa wakati, na ndani ya muda wa mkataba, ili kutatua kero kwa wananchi hasa kipindi cha mvua, na kwamba watatoa fursa za ajira kwa vijana wanaozunguka mradi huo.

Nao baadhi ya wananchi wa Magalata, wamesema barabara hiyo ni mbovu sana na imekuwa ikiwaathiri katika shughuli za kijamii na kiuchumi.

TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Lucy Mayenga (katikati) akishuhudia utiaji saini wa makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Gimagi-Magalata wilayani Kishapu kati ya TARURA (kushoto) na Mkandarasi (kulia).
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Lucy Mayenga (katikati) akishuhudia utiaji saini wa makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Gimagi-Magalata wilayani Kishapu kati ya TARURA (kushoto) na Mkandarasi (kulia).
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Lucy Mayenga (katikati) akishuhudia utiaji saini wa makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Gimagi-Magalata wilayani Kishapu kati ya TARURA (kushoto) na Mkandarasi (kulia).
Kaimu Meneja wa TARURA wilaya ya Kishapu Mhandisi Hussein Shaweji (kushoto) akikabdhiana nyaraka na Mkandarasi Asha Said Hamdani mara baada ya kumaliza kutia saini makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa barabara kiwango cha Changarawe kutoka Gimagi hadi Talaga.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Lucy Mayenga akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Lucy Mayenga akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Lucy Mayenga akizungumza.
Diwani wa Kata ya Mwamalasa Bushi Mpina akizungumza.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Seth Msangwa akizungumza.
Kaimu Katibu wa CCM wilaya ya Kishapu Ally Shiganga akizungumza.
Kaimu Meneja wa TARURA wilaya ya Kishapu Mhandisi Hussein Shaweji akizungumza.
Mkandarasi Asha Said Hamdani akizungumza.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464