
Tanzania na Misri zimeendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliodumu kwa miaka 62, huku ziara ya kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Abdel Fattah El-Sisi, nchini Tanzania ikitajwa kuwa hatua muhimu ya kuendeleza ushirikiano huo.
Katika mazungumzo yaliyofanyika, pande zote mbili zilikubaliana kuongeza ushirikiano katika sekta za kimkakati zikiwemo biashara na uwekezaji, kilimo, uchukuzi, afya, elimu na nishati.
Aidha, Tanzania na Misri zimesaini hati mbili za makubaliano ya ushirikiano na zimekubaliana kuanzisha Jukwaa la Biashara litakalolenga kuongeza fursa za kiuchumi na kuimarisha ustawi wa wananchi wa nchi hizo mbili.
Serikali ya Tanzania pia imeeleza kuwa mawaziri na wataalamu wameelekezwa kuhakikisha makubaliano yote yaliyofikiwa yanatekelezwa kwa wakati na kwa ufanisi ili wananchi wanufaike na ushirikiano huo.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464