` JUKWAA LA VIONGOZI WANAWAKE WAFURAHISHWA NA MARIDHIANO

WANDAMAN HOTEL

JUKWAA LA VIONGOZI WANAWAKE WAFURAHISHWA NA MARIDHIANO

Jukwaa la Viongozi Wanawake nchini (WLF) limesema amani, umoja na maridhiano ya kisiasa ni msingi wa maendeleo ya taifa, likiwataka Watanzania kuweka maslahi ya nchi mbele kuliko tofauti za kisiasa.

Makamu Mwenyekiti wa WLF, Azza Haji Suleiman, amesema usalama wa Zanzibar una mchango mkubwa katika kuimarisha usalama wa Muungano, akisisitiza umuhimu wa mshikamano wa wananchi.

WLF imesema utulivu wa kisiasa huwezesha uwekezaji, ajira na ukuaji wa uchumi, huku ikitaka ushindani wa kisiasa ubaki kwenye sanduku la kura na vyama kushirikiana katika masuala ya maendeleo.

Jukwaa hilo limepongeza hatua ya viongozi wa CCM na ACT-Wazalendo kusaini Tamko la Pamoja la Mwafaka wa Kisiasa Zanzibar, likisema kulinda amani ni jukumu la kila Mtanzania.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464