` VIONGOZI WA UWT WASHAURIWA KUDUMISHA UMOJA NA UPENDO

WANDAMAN HOTEL

VIONGOZI WA UWT WASHAURIWA KUDUMISHA UMOJA NA UPENDO



Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha  baraza

Na Suzy Butondo, Shinyanga

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Rehema Nhamanilo, amewashauri makatibu, wenyeviti wa UWT wa kata pamoja na madiwani kuachana na makundi ya uchaguzi na badala yake kuendelea kushirikiana katika kutekeleza shughuli za chama.

Nhamanilo ametoa ushauri huo katika kikao cha kawaida cha Baraza la UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini, ambapo aliwashauri viongozi hao kuweka mbele maslahi ya jumuiya na chama kwa kufanya kazi kwa umoja na uwajibikaji.

"Niwaombe sana madiwani wangu wa viti maalumu na viongozi wote muendelee kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha mnafanya vikao vyenu kwa wakati., pia ongezeni kasi ya usajili wa wanachama wa UWT kwani bado wapo wengi wanaohitaji kusajiliwa, hivyo ni muhimu kuwafikia," amesema Nhamanilo.

Ameongeza kuwa viongozi wanapaswa kuendelea kudumisha upendo na kuheshimiana ili kuepusha migogoro inayoweza kudhoofisha mshikamano ndani ya jumuiya.

"Tuendelee kudumisha upendo wetu na kuheshimiana. Tukifanya hivyo, tutaepusha migogoro ya aina yoyote na kuendelea kusonga mbele katika umoja wetu," ameongeza.

Kwa upande wake, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga, Hamisa Chacha, amewataka viongozi wa UWT Shinyanga Mjini kuendelea kufanya vikao vya kata na kuhakikisha shughuli zote za chama zinatekelezwa kwa ufanisi.

"Viongozi muwe wabunifu katika kutekeleza majukumu yenu na mshirikiane na madiwani wa viti maalumu kuhamasisha wanachama kulipa ada zao kwa wakati. Kila mmoja anapaswa kutimiza wajibu wake ndani ya jumuiya yake," amesema Chacha.
Amesisitiza kuwa ushirikiano, ubunifu na uwajibikaji miongoni mwa viongozi ni muhimu katika kuimarisha chama na jumuiya zake.


Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha  baraza

Katibu wachama cha mapinduzi CCM Shinyanga mjini  Hamisa Chacha akizungumza kwenye kikao cha baraza 
l
Kaimu katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Naibu Katalambula akizungumza 














Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464