` MBUNGE ASIFU AMANI YA TANZANIA

WANDAMAN HOTEL

MBUNGE ASIFU AMANI YA TANZANIA

MBUNGE wa Jimbo la Kahama Mjini, Benjamin Ngayiwa, amesema Tanzania ni nchi ya mfano kutokana na amani na utulivu inayodumu, wakati nchi nyingine zikikumbwa na migogoro.
Akizungumza kuhusu hali ya amani nchini, Ngayiwa amebainisha kuwa mataifa mengine bado yanashuhudia vita vya wenyewe kwa wenyewe pamoja na migogoro ya kidini, kikabila na kimkoa.
“Tunashuhudia katika maeneo mengine vita vya wenyewe kwa wenyewe lakini na migogoro ya kidini, yakikabila, yakimaeneo inakuwepo. Lakini Tanzania tunamshukuru Mungu na wananchi kwa ujumla, na jitihada za serikali katika kuitunza amani,” amesema Ngayiwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464