` "MATUSI NO, HOJA NDIO!" KIHONGOSI AWASHA MOTO IRINGA,AWATOLEA NJE WANASIASA WANAOHUBIRI VURUGU MTANDAONI NA UWANJANI

WANDAMAN HOTEL

"MATUSI NO, HOJA NDIO!" KIHONGOSI AWASHA MOTO IRINGA,AWATOLEA NJE WANASIASA WANAOHUBIRI VURUGU MTANDAONI NA UWANJANI

 

Msemaji Mkuu wa Chama Cha Maapinzui (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi amezichanga karata zake upya na kuweka nukta kwenye siasa za drama na taharuki nchini, akiwataka wanasiasa wenzake kushuka uwanjani kwa hoja za maendeleo badala ya kutafuta 'kiki' zinazohatarisha amani ya nchi.

Akizungumza kwa hisia kali mbele ya umati wa wananchi waliofurika katika Uwanja wa Mwembetogwa mkoani Iringa, Kihongosi ameweka wazi kuwa zama za siasa za kubomoa zimepitwa na wakati na sasa ni zamu ya kujibu hoja kwa hoja katika mazingira ya kuheshimiana. 

Katibu huyo wa Uenezi amewatupia dongo wale wote wanaotumia majukwaa mbalimbali, ikiwemo nguvu ya mitandao ya kijamii, kuchochea mgawanyiko na kusisitiza kuwa yeye yuko tayari wakati wowote kushiriki mijadala ya wazi itakayofunua nani ana nia ya kujenga na nani anataka kubomoa taifa.

Huku kauli zake zikisambaa kwa kasi mtandaoni na kuzua mijadala, Kihongosi ameshuka hadi ngazi ya chini kabisa kwenye kikao cha Shina Namba Kumi Kata ya Kihesa na kuwapa ujumbe mzito wazazi na vijana ambao ndio waathirika wakuu wa kampeni za hashtag na maandamano yasiyo na tija. 

Ujumbe wake uliokwenda viral ulikuwa wa wazi; kila mzazi ana wajibu wa kulinda mtoto wake na kila kijana ana wajibu wa kulinda wilaya yake dhidi ya kutumika kama chambo cha ajenda za siri zinazotaka kuivuruga Afrika, kwani wa kuipenda na kuilinda Tanzania ni Watanzania wenyewe. 

Alisisitiza kuwa badala ya vijana kuingizwa barabarani kupoteza nguvu kazi, nguvu hiyo ielekezwe kwenye malezi bora na kuviendeleza vipaji vyao mapema ili kuwandaa kuwa viongozi na wataalamu wa kesho.

Kihongosi amemaliza ziara yake ya kikazi mkoani Iringa kwa vitendo vinavyothibitisha maana halisi ya siasa za maendeleo anazohubiri baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Nduli. 

Mradi huo mkubwa uliogharimu kiasi cha Shilingi milioni 529.5 unalenga kuwakomboa na kuwapatia mazingira bora ya kusomea wanafunzi 820 wa eneo hilo, hatua inayozidi kuweka uzito kwenye kauli yake kuwa maendeleo ya wananchi ndio siasa halisi inayotakiwa na taifa kwa sasa na sio malumbano yasiyo na tija.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464