Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Bonge la Wakala uliofanyika leo Juni 25, 2026 mjini Shinyanga.
**
Na Kadama Malunde - Shinyanga
Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi imezindua rasmi kampeni ya “Bonge la Wakala”, kampeni maalumu inayolenga kuongeza kasi ya huduma za kifedha kupitia mawakala huku ikitoa mamilioni ya shilingi na zawadi mbalimbali kwa mawakala, wateja pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Kampeni hiyo inatekelezwa baada ya kuzinduliwa kitaifa jijini Mwanza hivi karibuni ikiwa sehemu ya mkakati mpana wa Benki ya CRDB wa kuimarisha ujumuishaji wa kifedha, kusogeza huduma karibu na wananchi na kuwapa motisha wadau wake wakuu wanaochangia ukuaji wa huduma za benki nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga leo Juni 25, 2026, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, amesema kampeni hiyo ni fursa adhimu kwa mawakala kuongeza miamala, kukuza biashara zao na kujiongezea kipato kupitia kamisheni na zawadi mbalimbali.
“Sasa tunapita kila kanda baada ya uzinduzi wa kitaifa. Hii ni fursa kubwa kwa mawakala wetu. Kinachotakiwa ni Kukimbiza Miamala 'Kuongeza miamala kwa wingi', kwani mbali na kamisheni mnazopata kila siku, sasa kuna zawadi nyingi zaidi zinazowasubiri,” amesema Wagana.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana.
Amesema mawakala wamekuwa nguzo muhimu katika mafanikio ya Benki ya CRDB kwa kusaidia kuwafikishia wananchi huduma za kifedha karibu na maeneo yao na hivyo kupunguza foleni katika matawi ya benki.
“Mawakala mnafanya kazi kubwa sana. Leo huduma za benki zimehamia mtaani na vijijini kupitia nyinyi. Mnaisaidia CRDB kuwahudumia wateja kwa haraka na ufanisi. Tunawashukuru kwa mchango wenu mkubwa ulioifanya CRDB kuendelea kuwa benki kinara Tanzania na hata nje ya mipaka ya nchi,” ameongeza.
Kwa upande wake, Meneja wa Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Anselm Mwenda, amesema kampeni hiyo imebuniwa ili kuongeza ushindani chanya miongoni mwa mawakala na kuwahamasisha kutumia kikamilifu fursa zilizopo katika huduma za wakala.
“Mawakala wamekuwa mabalozi wetu wakubwa katika kuwafikishia wananchi huduma za kifedha. Tunawaomba waichangamkie kampeni hii kwa kuongeza miamala na kuwahudumia wateja wengi zaidi ili waweze kunufaika na zawadi zilizotengwa,” amesema Mwenda.
Akitoa maelezo kuhusu kampeni hiyo, Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Kidagaa Peter Kubalunga, amesema kampeni ya Bonge la Wakala itanufaisha makundi yote muhimu yanayochangia ukuaji wa huduma za benki, yakiwemo wateja, mawakala, wafanyakazi wa benki na Mawakala Wakuu (Super Agents), kupitia zawadi mbalimbali zitakazotolewa kila wiki, kila mwezi, kila robo mwaka pamoja na zawadi kubwa za mwisho wa kampeni, zikiwa na lengo la kuongeza matumizi ya huduma za kibenki, kukuza miamala na kuwazawadia wadau wanaofanya vizuri zaidi.
Amesema kwa upande wa wateja, kila wiki wateja 33 watashinda Sh20,000 kila mmoja, huku kila mwezi washindi 11 kutoka kila kanda wakijinyakulia simu janja.
Aidha, kila robo mwaka mshindi mmoja atapata friji kubwa aina ya Double Door Fridge na washindi 10 watapata runinga za kisasa za Smart TV zenye ukubwa wa inchi 65.
Katika zawadi kubwa za mwisho wa kampeni, mshindi wa kwanza atajishindia Sh milioni 30, mshindi wa pili Sh milioni 20 na mshindi wa tatu Sh milioni 10.
Kubalunga amesema mawakala nao hawajaachwa nyuma kwani kila mwezi kutakuwa na bonasi za kamisheni kwa mawakala watakaofikia malengo ya miamala kwa asilimia 100, simu janja kwa wakala bora katika kila kanda pamoja na zawadi ya Sh30,000 kwa mawakala wenye miamala hai zaidi ya 30.
Kila robo mwaka mawakala watatu bora katika kila kanda watajishindia pikipiki, huku washindi wengine 10 wakipata mashine za POS. Aidha, zawadi kubwa ya Sh. milioni 10 imetengwa kwa wakala atakayeonyesha ukuaji mkubwa zaidi wa biashara katika kila kanda.
Kwa upande wa wafanyakazi wa Benki ya CRDB na Mawakala Wakuu (Super Agents), Kubalunga amesema kila mwezi matawi bora katika kila kanda yatapata jumla ya Sh milioni 1 ambapo mshindi wa kwanza atapata Sh500,000, mshindi wa pili Sh300,000 na mshindi wa tatu Sh200,000.
Pia kila robo mwaka kutakuwa na zawadi ya Sh milioni 5 kwa Meneja Bora wa Mahusiano ya Kanda (ZRM). Kwa Super Agents, watakaofikia zaidi ya asilimia 100 ya malengo watajishindia Sh milioni 10, watakaofikia zaidi ya asilimia 90 watapata Sh milioni 5, huku watakaofikia zaidi ya asilimia 80 wakijishindia Sh milioni 3.
Kubalunga amesema kampeni hiyo inaonesha namna ambavyo Benki ya CRDB inaendelea kuwekeza kwa wadau wake na kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha za kidigitali, sambamba na mkakati wa benki wa kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
Kampeni hiyo pia inaendana na juhudi za CRDB za kuimarisha ubunifu, huduma za kisasa na ujumuishaji wa kifedha nchini.
Amesema ushindi katika kampeni hiyo utategemea bidii ya washiriki katika kufanya miamala na kutumia huduma za CRDB Wakala, huku akisisitiza kuwa kila wakala na mteja ana nafasi sawa ya kuibuka mshindi.
“Bonge la Wakala siyo kampeni ya kawaida. Ni kampeni ya kuwathamini wale wote wanaoshiriki kukuza huduma za kifedha nchini. Tunawaalika wananchi, mawakala na wafanyakazi wa CRDB kuitumia kikamilifu fursa hii ya kipekee,” amesema Kubalunga.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Bonge la Wakala uliofanyika leo Juni 25, 2026 mjini Shinyanga.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Bonge la Wakala uliofanyika leo Juni 25, 2026 mjini Shinyanga.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Bonge la Wakala uliofanyika leo Juni 25, 2026 mjini Shinyanga.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Bonge la Wakala uliofanyika leo Juni 25, 2026 mjini Shinyanga.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Bonge la Wakala uliofanyika leo Juni 25, 2026 mjini Shinyanga.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Bonge la Wakala uliofanyika leo Juni 25, 2026 mjini Shinyanga.

Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Kidagaa Peter Kubalunga, akitoa maelezo kuhusu Kampeni ya Bonge la Wakala wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika leo Juni 25, 2026 mjini Shinyanga.

Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Kidagaa Peter Kubalunga, akitoa maelezo kuhusu Kampeni ya Bonge la Wakala wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo

Meneja wa Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Anselm Mwenda, akizungumza na mawakala wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Bonge la Wakala

Meneja wa Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Anselm Mwenda, akizungumza na mawakala wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Bonge la Wakala

Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Bonge la Wakala uliofanyika leo Juni 25, 2026 mjini Shinyanga.

Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Bonge la Wakala uliofanyika leo Juni 25, 2026 mjini Shinyanga.