` MPANGO WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI MKOMBOZI WILAYANI KISHAPU

WANDAMAN HOTEL

MPANGO WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI MKOMBOZI WILAYANI KISHAPU

 

Na Marco Maduhu, KISHAPU.

MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, wamesema mradi wa mpango wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi unaokwenda kutekelezwa wilayani humo, utakuwa mkombozi mkubwa katika kukabiliana na changamoto ya ukame.

TAZAMA VIDEO 👇👇


Wamebainisha hayo leo Juni 26, 2026 wakati wa Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani, uliolenga kupokea uwasilishwaji wa mpango kazi wa jamii wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, utakaotekelezwa katika kata 10 za halmashauri hiyo.
Akizungumza kwenye mkutano huo, mmoja wa madiwani ambao mradi huo unatekelezwa kwenye maeneo yao, Bujiku Mganganyanda wa Mwaweja, amesema wameupokea mradi huo kwa mikono miwili ambao unakwenda kutatua changamoto ya muda mrefu ya uhaba wa mvua na ukame uliokuwa ukiathiri shughuli za kiuchumi.

"Tumeupokea mradi huu kwa mikono miwili, kishapu tumekuwa na changamoto ya ukame kwa muda mrefu, lakini tuna imani kupitia mpango huu tunakwenda kuondokana na hali hii," amesema Mganganyanda.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Enock Rubeni, amewataka madiwani ambao mradi huo unapita kwenye maeneo yao wakausimamie ipasavyo, sababu wanaimani mradi huo unakwenda kuleta mabadiliko makubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi, amesema wilaya hiyo ni kame, na kusisitiza kupitia mradi huo, wananchi wapande miti kwa wingi, ili wapate mvua na kuondokana na hali ya ukame.
Akiwasilisha mchanganuo wa mpango huo, Mratibu wa Programu ya Scale Wilaya ya Kishapu Revocatus Mboya, amesema ni wa miaka mitano kuanzia 2026–2030.

Amefafanua kuwa, utekelezaji wake utatumia mfumo wa 'Lipa kwa Matokeo' (Payment for Results), chini ya usimamizi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ufadhili wa Benki ya Dunia (WB).
Aidha, ametaja shughuli ambazo zitafanyikwa kwenye mpango huo kuwa ni uchimbaji wa mabwawa ya maji, upandaji miti, miradi ya utengenezaji mkaa mbadala, utoaji wa mbegu bora za mazao za kustahimili ukame, na mbegu bora za mifugo aina ya borani, na malengo yake ni kuongeza kipato na utunzaji wa mazingira.

Kata 10 ambazo zinatekelezewa mradi huo ni Masanga, Mwamalasa, Somagedi, Shangihilu, Ndoleleji, Lagana, Ngofila, Kiloleli, Mwaweja na Mwakipoya.

MAELEZO KATIKA PICHA👇👇
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi akizungumza.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Josephat Limbe akizungumza.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Enock Ruben.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Emmanuel Jonson akizungumza.
Kaimu Katibu wa CCM wilaya ya Kishapu Rejina Ndulu akizungumza.
Katibu Tawala Msaidizi Rasilimali watu na Utawala Mkoa wa Shinyanga Ibrahimu Makana akizungumza
Mratibu wa Programu ya Scale Wilaya ya Kishapu Revocatus Mboya akiwasilisha mpango huo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi wilayani humo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464