` MPANGO WA KUTOKOMEZA UKATILI WAZINDULIWA KIJIJI CHA SAYU WILAYANI SHINYANGA

WANDAMAN HOTEL

MPANGO WA KUTOKOMEZA UKATILI WAZINDULIWA KIJIJI CHA SAYU WILAYANI SHINYANGA

MPANGO WA KUTOKOMEZA UKATILI WAZINDULIWA KIJIJI CHA SAYU WILAYANI SHINYANGA

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MPANGO shirikishi na endelevu wa utoaji wa elimu ya afya ya jamii na kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na makundi maalumu, umezinduliwa rasmi katika Kjiji cha Sayu Kata ya Pandagichiza wilayani Shinyanga.

TAZAMA VIDEO👇👇
Katika uzinduzi huo ambao umefanyika leo Juni 25, 2026, imebainika kuwa ukatili wa kijinsia umechukua sura mpya katika Kijiji cha Sayu, ambapo akina mama wamebuni mbinu ya kulala wakiwa wamevaa suruali ngumu za jinsi (jeans) kwa makusudi ya kuwanyima waume zao unyumba.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo Mtendaji wa Kijiji cha Sayu ambaye pia alikuwa Kaimu Mtendaji wa Kata ya Pandagichiza Rwambo Mayanzani, amesema kuwa hapo awali wahanga wakubwa wa ukatili walikuwa ni wanawake na watoto, lakini hivi sasa upepo umebadilika ambapo wanaume wamekuwa wahanga wakubwa wa kunyimwa haki zao za ndoa.

“Hapo awali kabla ya elimu ya ukatili kutolewa wahanga wakubwa walikuwa wanawake na watoto, lakini hali imebadilika, ambapo watu wanaonyanyasika kwa kiasi kikubwa kwa sasa ni wanaume, ikiwamo kunyimwa unyumba na wake zao,” amesema Mayanzani.
Naye Mwenyekiti wa umoja wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Shinyanga yanayopambana na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (SHY-EVAWC Working Group), Jonathan Manyama, amesema vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia vinapaswa kupingwa na watu wote na kuacha tabia ya kufanyiana ukatili.

Manyama aliwasihi wananchi wa Kijiji cha Sayu, kushiriki kikamilifu katika mpango huo mpya ili kutokomeza vitendo hivyo vya ukatili.
Kwa upande wake, Mwanzilishi wa mpango huo Shadrack Dase, amesema aliamua kuanzisha mradi huo baada ya kuguswa na kuongezeka kwa matukio ya ukatili ndani ya jamii, akiamini kuwa elimu hiyo itasaidia kuboresha ustawi wa wananchi.

Nao baadhi ya wananchi wa kijiji hicho, akiwamo Verena Mihambo, wamesema mradi huo umefika kwa wakati muafaka kwa sababu masuala ya ukatili bado yapo, hasa ya watoto wa kike kuolewa chini ya umri wa miaka 18 na unyanyasaji wa wazee. Mihambo ametumia pia fursa hiyo kuwaasa wanawake wenzake kuacha tabia ya kuwanyima unyumba waume zao.
Nao baadhi ya wananchi akiwamo Verena Mihambo, amesema mradi huo wameupokea na utawasaidia kwenye kijiji hicho sababu ukatili bado, hasa ukatili wa watoto kuolewa chini ya umri wa miaka 18, pamoja na wazee kunyanyaswa ikiwamo kunyimwa unyumba, na kuwasihi wanawake wasiwanyime waume zao tendo la ndoa.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Sayu Peter Luponya, amesema wameupokea mradi huo kwa shangwe kubwa na wataupa ushirikiano wa kutosha, ili kuhakikisha vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia vinatokomezwa kabisa kijijini hapo.

MAELEZO KATIKA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa umoja wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Shinyanga yanayopambana na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (SHY-EVAWC Working Group), Jonathan Manyama akizungumza.

Mtendaji wa Kijiji cha Sayu ambaye pia alikuwa Kaimu Mtendaji wa Kata ya Pandagichiza Rwambo Mayanzani akizungumza.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Pandagichiza Clara Michael akizungumza.
Mwanzilishi wa mpango wa kutokomeza vitendo vya ukatili Shadrack Dase akizungumza.
Mwanzilishi wa mpango wa kutokomeza vitendo vya ukatili Shadrack Dase akizungumza.
Uzinduzi wa mpango wa ukatili ukiendelea.
Uzinduzi wa mpango wa ukatili ukiendelea.
Uzinduzi wa mpango wa ukatili ukiendelea.
Uzinduzi wa mpango wa ukatili ukiendelea.
Uzinduzi wa mpango wa ukatili ukiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464