` UVCCM SHINYANGA YAWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI,KUDUMISHA AMANI

WANDAMAN HOTEL

UVCCM SHINYANGA YAWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI,KUDUMISHA AMANI



UVCCM SHINYANGA YAWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI,KUDUMISHA AMANI

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga, imewataka vijana wa umoja huo kufanya mikutano ya kusikiliza kero zinazowakabili vijana na kuzitafutia ufumbuzi, sambamba na kuwatangazia fursa mbalimbali za kiuchumi ili wajikwamue kimaisha.

TAZAMA VIDEO👇👇
Wito huo umetolewa leo Juni 24, 2026 na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Bernard Benson Werema, wakati wa kikao cha Baraza la UVCCM mkoani humo.

Werema amesema, vijana wa UVCCM ambao ni sehemu ya uongozi wa chama kinachoongoza Serikali, wanapaswa kuwahudumia vijana wote bila ubaguzi, kuwasikiliza changamoto zao na kuzifikisha katika mamlaka husika kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.

"Vijana wa UVCCM tuna wajibu wa kuwasikiliza vijana wote bila kuwabagua, kutatua changamoto zao na kuwatangazia fursa mbalimbali za kiuchumi, ili waweze kujikwamua na kuboresha maisha yao," amesema Werema.
Pia, amewataka vijana kuendelea kudumisha amani na utulivu wa nchi. ili shughuli za maendeleo ziendelee kufanyika kwa mazingira salama.

"Amani ndiyo msingi wa maendeleo, tunapaswa kuilinda na kuidumisha ili Taifa letu liendelee kuwa na utulivu na maendeleo ya wananchi yaendelee kupatikana," ameongeza Werema.
Kwa upande wake, Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Odilia Batimayo, amewataka vijana kuendelea kukijenga chama na kuwa na ndoto ya kuwa viongozi wakubwa wa baadaye, huku akiwahimiza kujiepusha na makundi yasiyo na tija ndani ya chama.

"Vijana mjijenge ndani ya chama na muwe na maono ya kuwa viongozi wa kesho. Epukeni makundi yasiyo na tija ambayo yanaweza kudhoofisha mshikamano wa chama," amesema Batimayo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, amewapongeza vijana hao kwa kazi kubwa wanayoifanya, na kusema kuwa ni jeshi muhimu la Chama Cha Mapinduzi.

"Nawapongeza vijana wa UVCCM kwa kazi kubwa mnayoifanya na kwa namna mnavyofuatilia fursa zilizopo katika Mkoa wa Shinyanga, Serikali itaendelea kushirikiana nanyi katika kuhakikisha vijana wananufaika na fursa hizo," amesema Mhita.
 
Mhita ameahidi ushirikiano wa kutosha kwa vijana hao, katika juhudi za kuwainua kiuchumi na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya mkoa.

MAELEZO KATIKA PICHA👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Bernard Benson Werema akizungumza.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Bernard Benson Werema akizungumza.
Katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Salama Mhampi akizungumza.
Katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Salama Mhampi akizungumza.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464