` UPANUZI WA BANDARI YA DAR ES SALAAM: GATI 10 MPYA NA MIUNDOMBINU YA UBARIDI KUWEZESHA USAFIRISHAJI WA MAZAO YA MBOGAMBOGA

WANDAMAN HOTEL

UPANUZI WA BANDARI YA DAR ES SALAAM: GATI 10 MPYA NA MIUNDOMBINU YA UBARIDI KUWEZESHA USAFIRISHAJI WA MAZAO YA MBOGAMBOGA



Serikali ya Awamu ya Sita imezindua mfumo wa 'Hifadhi Skimu' kupitia Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) uliolenga kuleta mageuzi katika mfumo wa hifadhi ya jamii kwa kuwajumuisha wananchi waliojiajiri katika mfumo rasmi wa kujiwekea akiba.
Mpango huo unatekelezwa chini ya miongozo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050, ukilenga kuwafikia mamilioni ya Watanzania wakiwemo wakulima, wafugaji, wavuvi, wachimbaji wadogo wa madini, pamoja na wajasiriamali wadogo kama waendesha bodaboda na mama lishe.

Kupitia Hifadhi Skimu, wananchi sasa watakuwa na uhakika wa maisha ya sasa na ya baadaye kwa kunufaika na mafao mbalimbali yakiwemo pensheni ya uzee, urithi, ulemavu, uzazi, na huduma za matibabu kupitia michango yao ya hiari.

Msemaji wa serikali akihimiza wananchi wajiunge na mfumo huo alisema kwamba ni rahisi kwani NSSF imeweka mfumo rahisi wa kujiandikisha na kuchangia kwa kutumia simu ya kiganjani kwa kupiga namba ya huduma 15200# na kufuata maelekezo rahisi

Hatua hii inalenga kuondoa dhana ya zamani kuwa hifadhi ya jamii ni kwa ajili ya watumishi wa sekta rasmi pekee, na badala yake kuwapa kinga ya kijamii wananchi wote wanaojituma katika kazi mbalimbali za uzalishaji mali.

Msemaji Mkuu wa Serikali amewahimiza wajasiriamali na waliojiajiri kuchangamkia fursa hii ya kipekee ili kujiwekea akiba itakayowasaidia kukabiliana na majanga pamoja na kuwa na maisha bora wakati wa uzee, huku Serikali ikiendelea kutumia rasilimali zilizopo kukuza uchumi na kutengeneza ajira kwa vijana nchi nzima.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464