` RIPOTI YA JAJI CHANDE INA HOJA MUJARABU TUSIIPONDE KWA KUFUATA MIKUMBO

WANDAMAN HOTEL

RIPOTI YA JAJI CHANDE INA HOJA MUJARABU TUSIIPONDE KWA KUFUATA MIKUMBO



Katika kile kinachoonekana kama msisitizo wa dhati wa kulinda uhuru na utu wa taifa, Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman ametoa wito mzito kwa Watanzania kuamini na kutumia mifumo yao ya ndani katika kutatua migogoro badala ya kukimbilia msaada kutoka kwa mataifa ya nje.


Jaji Chande amebainisha hayo hivi karibuni akitoa ufafanuzi jinsi ripoti yake iulivyofanyakazi na methodoliojia ya kisayansi iliyotumia kuypata majibu katika kadhia iliyoitia doa nchi hapo Oktoba 29 mwaka 2025.

Katika ufafanuzi wake alifundisha bayanakuwa dhana ya kutafuta wageni kuja kuingilia mivutano ya ndani ni ishara ya kutojiamini na kupuuza busara ambazo Watanzania wamezitumia kwa miongo mingi kudumisha utulivu.

Amesisitiza kuwa kama taifa hatujashindwana na tuna uwezo kamili wa kuketi meza moja na kumaliza tofauti zetu bila kuhitaji "macho ya nje" ambayo mara nyingi hayajui undani wa utamaduni na mshikamano wetu.

Uchambuzi wa ujumbe huo unaonesha kuwa amani ya kweli inajengwa juu ya msingi wa haki na usawa ambapo kila raia, bila kujali cheo chake, anapaswa kujiweka chini ya sheria.

Aidha, katika ripoti yake amesisitiza matumizi ya njia mbadala za kutatua migogoro kama vile usuluhishi na upatanishi ambazo hupunguza chuki na mivutano ndani ya jamii.

Amesisitiza kuwa Watanzania wanapaswa kuamini mifumo ya kisheria iliyopo kwani ndiyo njia pekee ya kulinda fahari ya nchi. Kwa mujibu wa Jaji Chande, uongozi wenye maono na hekima ni ule unaoweza kujifunza kupitia makosa ya nyuma na kuimarisha amani kama chaguo kuu la taifa, huku akihitimisha kuwa amani yetu ni fahari yetu na ni jukumu la kila mmoja wetu kuilinda kwa gharama yoyote.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464