` MIKOA YA KANDA ZIWA YAFIKIWA NA ELIMU UFUATILIAJI NA TATHIMINI KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

WANDAMAN HOTEL

MIKOA YA KANDA ZIWA YAFIKIWA NA ELIMU UFUATILIAJI NA TATHIMINI KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

 

Na Mwadishi wetu- Mwanza

Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuchukua hatua thabiti za kuimarisha mifumo ya usimamizi wa utendaji na uwajibikaji kwa kutoa Elimu Tathimini na Ufuatiliaji kwa Wataalam wa serikali ili kuleta maendeleo wananchi. 

Katika  juhudi hizo, viongozi na wataalam kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa wamekutana  leo tarehe 14 Mei, 2026 Mkoani Mwanza katika kikao kazi maalum kilichojumuisha Mikoa ya Mwanza, Kigoma, Geita, Simiyu, Kagera, Shinyanga na Marakwa lengo kuu ni kujadili na kuimarisha utekelezaji wa Mwongozo Jumuishi wa Ufuatiliaji na Tathmini.

Akimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonaz, Katibu Tawala  wa Mkoa wa Mwanza Ndugu Balandya Elikana, amewashukuru washiriki kwa kujitokeza katika kikao kazi ambacho ni sehemu ya mafunzo, maagizo ya Serikali ya kuunganisha nguvu na kutumia mbinu za pamoja katika Kufuatilia na Kupima Utendaji kazi wa sekta za umma.

Ameeleza kuwa licha ya serikali kuwa na miongozo kadhaa ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa mda mrefu, tathmini imeonesha kuna changamoto za kukosekana kwa uratibu na matumizi ya mifumo isiyounganishwa na kutegemea ufuatiliaji wa mchakato badala ya matokeo, pamoja na upungufu wa kufanya tathmini za mara kwa mara. Hali ambayo imeathiri upatikanaji wa taarifa sahihi kwa maendeleo ya Taifa.

”Hii ni fulsa kubwa ya kujifunza na kuelewa miongozo Mbalimbali ya Tathmini na Ufuatiliaji  kwa wataalam kutoka ngazi ya Mkoa na Halmashauri kwani Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu wametoa mafunzo haya kwa Wataalam katika Halmashauri nyingi nchini, kilichobaki ni kwetu sisi katika utekelezaji. Amesema Ndugu Balandya Elikana.

Aidha, amewakumbusha viongozi na wataalam majukumu yao kuhakikisha mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini unatekelezwa ipasavyo kwa kila Halmashauri.

Amewasisitiza Wakurugenzi wa Halmashauri kuimarisha vitengo vya Ufuatiliaji na Tathmini kwa kuviwezesha vitengo kuwa na rasilimali watu na fedha, huku Maafisa Mipango wakisisitizwa kuoanisha mipango na viashiria vinavyopimika tangu hatua za awali za miradi inayotekelezwa katika Halmashauri zao.

Pia ametumia fulsa hiyo kuwaalika wataalam hao katika wiki Ufuatiliaji na Tahmini Tanzani itakayofanyika tarehe 20 hadi 26 septemba 2026 Katika Ukumbi wa Ngurdoto Mauntain Jijini Arusha.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendeji wa Serikali  Bi. Sakina Mwinyimkuu, amesema Ufuatiliaji na Tathimini sio tu ufuatiliaji wa Miradi, bali ni mfumo wa kila siku wa maisha, hivyo ni lazima kupeana elimu ili kuweza kuelewana katika utekelezaji wa majukumu ya shughuli za serikali ili kuwasaidia wananchi katika kupata huduma.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464