` DIWANI MHANDISI JUMANNE RAJABU AZINDUA MPANGO WA CHAKULA SHULENI KATA YA PUNI KIUNUA TAALUMA

WANDAMAN HOTEL

DIWANI MHANDISI JUMANNE RAJABU AZINDUA MPANGO WA CHAKULA SHULENI KATA YA PUNI KIUNUA TAALUMA

 



Na Marco Maduhu, SHINYANGA

DIWANI wa Kata ya Puni wilayani Shinyanga Mhandisi Jumanne Rajabu, amezindua rasmi mpango wa ulaji chakula katika shule zote za kata hiyo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuinua kiwango cha taaluma kwa wanafunzi.

VIDEO👇

Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 11, 2026 katika Shule ya Msingi Buyubi, ambapo diwani huyo alikabidhi gunia nne za mahindi na maharage pamoja na Sh.200,000 kwa ajili ya kuanzisha mpango huo.
Amesema ulaji wa chakula shuleni ni muhimu kwa wanafunzi, kwa kuwa utawasaidia kuzingatia masomo yao na kufanya vizuri kitaaluma tofauti na kusoma wakiwa na njaa.

Aidha, amesema katika shule hiyo ya Buyubi pia ametoa kompyuta na printer, vifaa vitakavyosaidia kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Buyubi, Amiri Sendoro, amesema mpango huo wa chakula utasaidia kuongeza kiwango cha taaluma kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Naye Afisa Elimu wa Kata ya Puni, Martine Kingu, amewataka wazazi kuunga mkono mpango huo kwa kuchangia chakula shuleni ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
Mmoja wa wazazi, Hamisa Yusuph, amesema wamehamasika kuchangia chakula shuleni, ili watoto wao wasome kwa bidii na kuwasikiliza walimu.

Baadhi ya wanafunzi akiwamo Sabina Peter, wamesema wanaushukuru mpango huo wa chakula kuanzishwa shuleni hapo kwa kuwa utawasaidia kusoma kwa bidii na kufanya vizuri katika masomo yao.

TAZAMA PICHA👇👇
Diwani wa Puni Mhandisi Jumanne Rajabu akizungumza.
Diwani wa Puni Mhandisi Jumanne Rajabu akikabidhi magunia ya Mahindi na Maharage.
Diwani wa Puni Mhandisi Jumaane Rajabu akikabidhi Computer na Printer.
Diwani wa Puni Mhandisi Jumanne Rajabu akizungumza na wanafunzi.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464