` SKAUTI KUWAFUNDISHA VIJANA WILAYANI NZEGA KUWA RAIA WEMA NA WENYE UZALENDO NA NCHI YAO

WANDAMAN HOTEL

SKAUTI KUWAFUNDISHA VIJANA WILAYANI NZEGA KUWA RAIA WEMA NA WENYE UZALENDO NA NCHI YAO


Na Marco Maduhu, NZEGA

Vijana waliopo kwenye kambi ya mafunzo ya Skauti wilayani Nzega mkoani Tabora, wamesema mafunzo hayo yanawafundisha kuwa wakakamavu na wazalendo katika nchi yao.

TAZAMA VIDEO👇👇
Wamebainisha hayo jana wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, yaliyofunguliwa na Mgeni Rasmi Afisa Tarafa ya Puge, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Naitapwaki Tukai.
Mmoja wa vijana hao Ramadhani Juma, amesema wapo kambini hapo kujifunza mazoezi mbalimbali ya ukakamavu na kuwa wazalendo, na kwamba mafunzo hayo yanawasaidia katika maisha yao ya baadaye.

Naye Kamishina Msaidizi wa Skauti wilayani Nzega Beatus Jumanne, amesema malengo ya skauti ni kuwalea vijana ili wawe wazalendo na wenye kuipenda nchi yao, na kwamba kambi hiyo ina jumla ya vijana 541, wavulana 330 na wasichana 221.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Tarafa ya Puge Rahma Mnyone, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Nzega, amesema skauti ni chama ambacho ni nguzo imara ya kujenga uzalendo, kujiamini, nidhamu, pamoja na kuwafanya vijana kuwa raia wema katika nchi yao na kuwasihi vijana hao wajifunze kwa uadilifu mkubwa.

MAELEZO KATIKA PICHA👇👇
Mgeni Rasmi Afisa Tarafa ya Puge Rahma Mnyone akizungumza.
Kamishina Msaidizi wa Skauti wilayani Nzega Beatus Jumanne akisoma taarifa kwa mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akivalishwa skafu.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464