` RPC SHINYANGA : MPIGA PICHA OFISI YA MKUU WA MKOA BOAZI MARTINE AMEFARIKI DUNIA, SABA AKIWEMO MWANDISHI WA ITV WAMEJERUHIWA

WANDAMAN HOTEL

RPC SHINYANGA : MPIGA PICHA OFISI YA MKUU WA MKOA BOAZI MARTINE AMEFARIKI DUNIA, SABA AKIWEMO MWANDISHI WA ITV WAMEJERUHIWA


RPC SHINYANGA : MPIGA PICHA OFISI YA MKUU WA MKOA BOAZI MARTINE AMEFARIKI DUNIA, SABA AKIWEMO MWANDISHI WA ITV WAMEJERUHIWA

Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi, kulia aliyevaa kofia ni Boazi Martine enzi za uhai wake
Eneo la ajali


Na Kadama Malunde - Shinyanga


Mpiga picha wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Boaz Martine amefariki dunia huku waandishi wa habari Frank Mshana wa ITV/Radio One na Johnson James wakiwa miongoni mwa watu saba waliojeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea Mei 19, 2026 katika Kata ya Samuye, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga.


Ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Toyota Harrier lenye namba T.210 EDB na Toyota Land Cruiser Hardtop lenye namba DFPA 8920 mali ya shirika la KOICA, lililokuwa limebeba waandishi wa habari pamoja na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 20, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Toyota Harrier aliyekuwa akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari, hali iliyosababisha kugongana na Land Cruiser hiyo na kutumbukia mtaroni.


Mbali na Frank Mshana na Johnson James afisa habari ofisi ya mkuu wa Mkoa, majeruhi wengine ni Koplo Swahiba Msangi, Neema Madono (36), Rehema Edson (45), Shadia Omari (32) pamoja na dereva wa Land Cruiser Laurence Peter (34).


Majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.


Kamanda Magomi ametoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani huku akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi litachukua hatua za kisheria dhidi ya madereva watakaobainika kusababisha ajali kwa uzembe.



Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464