
Wakazi wa Kata ya Ndala na Masekelo wamesema kuwa uongozi wa Rais Samia umeleta matumaini mapya kwa wananchi kwa kuhimiza upendo, mshikamano na ushirikiano bila kujali tofauti zao.
“Tunampongeza Rais wetu kwa kuendeleza yale yaliyoasisiwa na viongozi wa mwanzo wa taifa letu. Umoja na amani ndiyo nguzo kuu ya maendeleo, na tunaona juhudi zake zina matokeo chanya" amesema Paulina.
Naye Alphonce Paul mkazi wa Kata ya Masekelo, amesema kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha anailinda na kuitunza amani iliyopo nchini kwa kushirikiana na serikali.
“Rais Samia anafanya kazi kubwa kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na utulivu. Sisi wananchi tunapaswa kumuunga mkono kwa vitendo, kwa kudumisha mshikamano na kuepuka migogoro isiyo ya lazima,”
mesema Alphonce.
Kwa upande wake, Jamila Athuman, mkazi wa Kata ya Ndala, amesisitiza kuwa amani ya Tanzania ni tunu adhimu inayopaswa kulindwa na kila kizazi.
“Amani tuliyonayo si ya bahati mbaya, ni matokeo ya misingi imara iliyowekwa na waasisi wetu. Ni wajibu wetu kuendeleza kwa kuunga mkono juhudi za Rais Samia,” amesema Jamila.
Wananchi hao wameeleza kuwa wana imani na uongozi wa Rais Samia katika kuendeleza dira ya taifa ya umoja, mshikamano na amani, wakihimiza Watanzania wote kushiriki kikamilifu katika kulinda tunu hizo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464