Na Sumai Salum- Kishapu
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi, amesema kuwa Wilaya hiyo imejipanga kikamilifu kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika Aprili 26, 2026 kimkoa wilayani humo ambapo Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Mboni Mhita akiwa ndiye mgeni rasmi.
Mhe. Masindi amesema maadhimisho hayo yataambatana na shughuli mbalimbali za kijamii zikiwemo zoezi la kufanya usafi wa mazingira Hospitali ya Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na kuwatembelea na kuwapa pole wagonjwa.
Aidha, ameeleza kuwa kutakuwa na uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ya awali katika Shule ya Msingi Isoso, hatua inayolenga kuboresha mazingira ya elimu kwa watoto wa eneo hilo.
Mbali na hilo, wananchi watapata fursa ya kushiriki michezo mbalimbali itakayofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Buduhe ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mshikamano na kuenzi Muungano.
Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Kishapu wameeleza kufurahishwa na ujio wa maadhimisho hayo wakisema ni fursa ya kipekee kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Baadhi ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ya Dkt. Jakaya Kikwete
Mwananchi ajulikanaye kwa jina la Guka Mgabo amesema huo ni wakati muhimu wa kujifunza historia ya nchi na kuthamini Muungano huo. Pia shughuli hizo zinawapa nafasi ya kushiriki katika maendeleo ya jamii kwa vitendo.
Naye Tina Shoka kutoka Kata ya Mwataga, Kijiji cha Migunga, amesema anajivunia kuona maadhimisho haya yanafanyika Wwilayani humo kwani hiyo ni fursa ya kuonyesha mshikamano na pia kuhamasisha maendeleo katika sekta ya elimu na huduma za jamii.
Kwa upande wake Natasha Donard amesema Maadhimisho hayo ni ukumbusho muhimu wa umoja kama Watanzania. Ni vyema kila mmoja kushiriki kikamilifu ili kuendeleza amani, upendo na mshikamano uliopo nchini.
Wananchi wote wanakaribishwa kushiriki kwa wingi katika maadhimisho hayo muhimu yatakayofanyika Aprili 26, 2026 katika Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, ili kwa pamoja kuuenzi na kuudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Miaka 62 ya Muungano yanaambatana na kauli mbiu isemayo "Amani, Umoja na Mshikamano ni Msingi wa maendeleo endelevu"

Sambamba na maandalizi ya ujio wa wageni kutoka kona zote za Mkoa wa Shinyanga kwenye maadhimisho hayo ya miaka 62 ya Muungano, Wananchi wa Kishapu leo Jumamosi ya Aprili 25,2026 wameendelea na zoezi la usafi wa kila mwisho wa mwezi kwa lengo la kuweka mazingira kuwa safi.PICHA ZA USAFI

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464