
Mwenyekiti wa kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Bw. Mabala Mlolwa amewaagiza viongozi wa chama na Serikali kushirikiana na watendaji wa serikali, Madiwani, venyeviti wa vijiji, mitaa na vitongiji na Madiwani kuhamasisha wananchi kujiunga na mpango wa bima ya Afya kwa wote.
Na Mwandishi wetu kutoka Mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya CCM mkoani Shinyanga ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM Bw. Mabala Mlolwa ameyasema hayo katika mkutano jumuishi wa kuhamasisha uhai wa chama na.kusikiliza kero za wananchi baada ya baadhi ya wananchi kuibua hoja ya kutokuwa na elimu sahihi ya kujiunga na Bima ya Afya kwa wote.
Kuhusu huduma za matibabu zinazopatikana kupitia bima hiyo, katibu muenezi wa CCM mkoa wa Shinyanga Richard Masele amesema mwananchi akishajiunga na bima hiyo anapata matibabu kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali za rufaa na za kitaifa ikiwemo Bugando na Muhimbili.
Mganga mfawishi wa kituo cha afya cha Old Shinyanga Dkt. amewahakikishia wananchi upatikanaji wa huduma bora za afya kupitia bina hiyo na kubainisha kuwa hadi sasa wagonjwa zaidi ya 50 wameshapatiwa matibabu tangu ziezi la uandikishaji lianze mnamo mwezi wa pili 2026.
Naye Diwani wa Kata ya Old Shinyanga Bw. Lucas Benedicto mgige amesema licha ya upatikanaji wa huduma bora katika vituo vya afya ikiwemo Old Shinyanga, bado upungufu wa wahudumu ni changamoto mtambuka na kuiomba serikaki kiliangalia jambo hilo kwa umakini mkubwa.
Akihitimisha ziara ya Kamati ya Siasa katika tarafa ya Shinyanga mjini, mwenyekiti Mabala Mlolwa amewataka viongozi wa chama na Serikali kujenga mazoea ya kushuka chini kwa wananchi kufanya mikutano shirikishi kupitia viongozi wa mashina au mabalozi wa nyumva 10 ili kuishirikisha jamii kujenga chama imara na chenye nguvu.