` MWENYEKITI HALMASHAURI YA KISHAPU AFANYA ZIARA SOMAGEDI, MWAKA WA FEDHA 2026/2027 NEEMA YA MIRADI YAJA

WANDAMAN HOTEL

MWENYEKITI HALMASHAURI YA KISHAPU AFANYA ZIARA SOMAGEDI, MWAKA WA FEDHA 2026/2027 NEEMA YA MIRADI YAJA

Na Sumai Salum- Kishapu


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Josephat Limbe, amesema kuwa katika mwaka wa fedha ujao 2026/2027 Halmashauri imejipanga kuhakikisha inakamilisha miradi yote iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi na kupitishwa kwenye bajeti hiyo kabla ya kuanza utekelezaji wa miradi mipya.


Mhe. Limbe ametoa kauli hiyo Aprili 28,2026 wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi katika Kata ya Somagedi, baada ya kupokea taarifa na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Wimate, iliyosomwa na Mtendaji wa Kijiji hicho, Joyce Mshiwi, mbele ya viongozi na watendaji wa Halmashauri.


"Kwanza kabisa tunamshukuru Rais wetu Mhe. Samia Suluhu kwa kuendelea kuleta fedha nyingi katika sekta ya afya, pili Mkurugenzi wetu Emmanuel Johnson ameendelea kuwa mtendaji mzuri na mtekelezaji wa maono ya serikali, sisi sote ni mashahidi wa ukamilishwaji wa miradi mingi hasa ya elimu na afya kupitia fedha za mapato ya ndani na serikali kuu na hapa ahadi yake ni kuwa atatekeleza na wote mtafurahia huduma bora za afya" amesisistiza Mhe. Mwenyekiti


Limbe emesema juhudi za ujenzi wa Zahanati hiyo yenye vyumba 19 lililogharimu kiasi cha Tsh. milioni 7,770,000 michango ya wananchi, mifuko 200 ya saruji kutoka kwenye mfuko wa jimbo na mifuko 50 ya saruji kutoka kwa Diwani wa Kata hiyo ni ishara tosha ya jamii hiyo kuwa na uhitaji wa huduma hiyo muhimu ya afya na Halmashauri itahakikisha wanapata fedha za ukamilishaji wa boma hilo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Josephat Limbe akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Wimate kata ya Somagedi wilayani humo na kusikiliza na kutatua kero za wananchi Aprili 28, 2026


Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo amesisitiza umuhimu wa lishe kwa wanafunzi, akimtaka Diwani wa Kata, Afisa Elimu wa Kata pamoja na Mtendaji wa Kata na vijiji kushirikiana na jamii kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanapata chakula wawapo shuleni.

“Nisisitize, msimu huu wa mavuno ndio muda mzuri wa kushirikiana na jamii kutoa elimu ya umuhimu wa chakula shuleni, na pia ni wakati sahihi wa kukusanya michango ya chakula na kukihifadhi kwa kuzingatia kanuni bora ili kidumu kwa muda mrefu,” amesema Mhe. Limbe.


Katika sekta ya elimu, imebainika kuwa kuna jengo katika Shule ya Msingi Imalabupina ambalo linahitaji fedha za ziada kutoka serikalini ili likamilike na kuanza kutumika.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Wimate Kata ya Somagedi wilayani
Kishapu mkoani Shinyanga Daniel Limbe akizungumza wakati wa ziara ya kikazi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Josephat Limbe ya kukagua mradi wa ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Wimate kata ya Somagedi wilayani humo na kusikiliza na kutatua kero za wananchi Aprili 28, 2026


Kwa upande wa kilimo na mifugo, Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri hiyo, Mwita Mwijarubi, amesema kuwa kiangazi kilichopita kilisababisha vifo vya jumla ya ng’ombe 35 katika Kata hiyo kutokana na ukosefu wa malisho na baadhi ya wafugaji kukataa kutoa mifugo yao ipate chanjo.

Diwani wa Kata ya Somagedi Mhe. Nyama Kisinza akisikiliza kwa makini maelekezo ya Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Josephat Limbe wakati wa ziara yake ya kikazi ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi Kijiji cha Wimate Aprili 28, 2026


“Serikali imeendelea kutoa chanjo za ruzuku kwa mifugo, lakini bado kuna baadhi ya wafugaji hawaitikii ipasavyo kutokana na dhana potofu. Tunaendelea kuwapa elimu ya utunzaji wa malisho na umuhimu wa kupunguza mifugo,” ameeleza Mwijarubi.

Akizungumzia suala la mikopo, Limbe amesema kuwa baadhi ya taasisi ndogondogo za kifedha (Microfinance) zimekuwa chanzo cha migogoro katika jamii, hali inayosababisha baadhi ya wananchi kukimbia makazi yao na kupoteza mali zao.


"Halmashauri kupitia kitengo cha sheria imeanza mapitio ya mikataba ya taasisi hizo, ambapo imeelekezwa kuwa katika miezi ya Aprili na Mei, taasisi hizo hazitaruhusiwa kutoa mikopo hadi zoezi la mapitio litakapokamilika mtafahamishwa" ameongeza.

Afisa Mtendaji wa kata ya Somagedi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Peter Deus akizungumza wakati wa ziara ya kikazi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Josephat Limbe ya kukagua mradi wa ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Wimate kata ya Somagedi wilayani humo na kusikiliza na kutatua kero za wananchi Aprili 28, 2026


Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii, Abednego Madole, amewahimiza Wananchi kutumia mikopo ya serikali inayotolewa kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ambayo haina riba, badala ya kukimbilia mikopo yenye masharti magumu kwa sababu ya kuogopa taratibu zilizowekwa kwenye mikopo ya serikali.


Hata hivyo, ameeleza kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa na mwitikio mdogo kutokana na taratibu zake, jambo linalowafanya kuchagua mikopo ya haraka ambayo baadhi yao imekuwa ikiwaumiza katika urejeshaji wake.


Mhe. Limbe ameongeza kuwa baada ya mapitio hayo, taasisi za fedha zitaruhusiwa kuendelea kutoa mikopo kwa kufuata taratibu mpya zitakazowekwa na Halmashauri, ikiwa ni pamoja na ushirikishwaji wa serikali za kata hadi ngazi ya vitongoji ili kulinda usalama wa wananchi.
Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, mifugo na uvuvi Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mwita Mwijarubi akizungumza wakati wa ziara ya kikazi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Josephat Limbe ya kukagua mradi wa ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Wimate kata ya Somagedi wilayani humo na kusikiliza na kutatua kero za wananchi Aprili 28, 2026


Aidha, amewataka maafisa maendeleo wa kata na wilaya kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu faida na athari za mikopo kabla ya kuichukua.


Diwani wa Kata ya Somagedi Mhe.Nyama Kisinza amepongeza na kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo za kuzungukia miradi na kusikiliza kero za wananchi kwa lengo la kuhakikisha jamii inapata huduma bora na kwa haraka.


"Mhe. Mwenyekiti nimepokea maelekezo yote uliyotuambia na tutayatekeleza n ahivyo kwanza kesho aprili 29, 2026 nitaanza rasmi ziara kwenye mashule yote nihakiishe lishe inazingatia ipasavyo lengo etuinue elimu yetu na watoto wapate mafanikio kupitia elimu hiyo" amesema Mhe. Kisinza

Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Abednego Madole akizungumza wakati wa ziara ya kikazi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Josephat Limbe ya kukagua mradi wa ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Wimate kata ya Somagedi wilayani humo na kusikiliza na kutatua kero za wananchi Aprili 28, 2026
Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Upendo Chiwango akizungumza wakati wa ziara ya kikazi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Josephat Limbe ya kukagua mradi wa ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Wimate kata ya Somagedi wilayani humo na kusikiliza na kutatua kero za wananchi Aprili 28, 2026
Muonekano wa nje wa jengo la Zahanati iliyojengwa na nguvu za wananchi wa Kijiji cha Wimate Kata ya Somagedi Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga na kuongezewa nguvu na mfuko wa jimbo na Diwani wa Kata hiyo

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Josephat Limbe (kushoto) na Diwani wa Kata ya Somagedi Mhe. Nyama Kisinza (kulia) wakiteta jambo baada ya kutoka kukagua boma la Zahanati ya Kijiji cha Wimate Kata ya Somagedi wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi huo na kusikiliza na kutatua kero za Wananchi Aprili, 28, 2026





































Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464