` MADRASA MSIKITI WA MUFTI ISSA SHABANI SIMBA WAKABIDHIWA MADAWATI, JUZUU NA MASAHAFU

WANDAMAN HOTEL

MADRASA MSIKITI WA MUFTI ISSA SHABANI SIMBA WAKABIDHIWA MADAWATI, JUZUU NA MASAHAFU



MADRASA MSIKITI WA MUFTI ISSA SHABANI SIMBA WAKABIDHIWA MADAWATI, JUZUU NA MASAHAFU

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Taasisi ya Mufti Simba imekabidhi madawati 30, Juzuu 540 na Masahafu 100, kwa madrasa katika msikitiki wa Mufti Issa Shabani Simba, uliopo Majengo ya zamani Manispaa ya Shinyanga.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Fatuma Simba, akizungumza wakati wa kukabidhi vitu hivyo, amesema katika kuenzi jina la aliyekuwa Mufti wa Tanzania Issa Shabani Simba, wameamua kuanzisha Taasisi ambayo itakuwa ikijihusisha na shughuli za kidini na kijamii katika Nyanja mbalimbali.
Amesema, wamefika katika Msikiti huo ambao uliasisiwa na Mufti huyo pamoja na kujenga Madrasa, ili kuboresha mazingira ya watoto kusoma kwenye mazingira rafiki, kwa kuwapatia madawati, juzuu na masahafu.

“Tumekabidhi madawati 30 katika madrasa ya msikiti wa huu wa Mufti Issa Shabani Simba, Juzuu na Masahafu, na baadhi ya Juzuu na Masahafu zitakwenda Kahama, lengo ni kuendelea kuenzi Jina la aliyekuwa Mfuti wa Tanzania Issa Shabani Simba,” amesema Fatuma.
Aidha, ametoa wito kwa wazazi na walezi wa dini ya kiislamu, kuwapeleka watoto wao kusoma madrasa ili kuwajenga katika misingi imara ya kidini na kuwa na maadili mema.

Naye Imamu Mkuu wa Msikiti wa Mufti Issa Shabani Simba Sheikh Balilusa Khamisi, amesema kuanzishwa kwa taasisi hiyo ya Mufti Simba ni jambo la kheli, sababu kutaenzi jina la aliyekuwa mufti huyo wa Tanzania kwa vitendo, kwa kufanya matendo mema ya kidini na kijamii.
Amesema, msikiti huo una vyumba vinne vya madrasa, na vyote vipo katika hali nzuri baada ya kuboreshwa na taasisi hiyo, na vina madawati ya kutosha pamoja na kuwapo kwa Juzuu na Masahafu.

Nao baadhi ya waumini wa dini hiyo akiwamo Alhaji Nurah Ngaramo, amesema msaada huo ni muhimu katika kuimarisha masomo ya madrasa kwa watoto, na kuwajenga wawe na maadili mema kupitia mafundisho ya kidini.

MAELEZO KATIKA PICHA👇👇
Imamu Mkuu wa Msikiti wa Mufti Issa Shabani Simba Sheikh Balilusa Khamisi akizungumza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mufti Simba, Yusuph Musun akizungumza.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mufti Simba, Fatuma Simba akielezea kuanzishwa kwa taasisi hiyo na msaada ambao wameutoa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mufti Simba, Yusuph Musun (kushoto) akimkabidhi madawati, Juzuu na Masahafu Imamu Mkuu wa Mskiti wa Mufti Issa Shabani Simba kwa ajili ya Madrasa ya Msikiti huo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464