.jpeg)
Baraza la Wafanyakazi la Nne la Tume ya Ushindani (FCC) limehitimisha kikao chake cha siku mbili kwa kuazimia kuunga mkono rasimu ya Mpango Mkakati Mpya wa Miaka Mitano 2026/27-2030/31 unaolenga kutekeleza moja kwa moja Dira ya Taifa ya 2050.
Kikao hicho kilichofanyika tarehe 9 na 10 Aprili, 2026 katika ukumbi wa Hoteli ya Sunset, Manispaa ya Morogoro kiliwakutanisha wajumbe wa Menejimenti na Wawakilishi wa Watumishi kujadili ajenda kuu mbili : Rasimu ya Mpango Mkakati na Rasimu ya Bajeti ya 2026/27
Akifunga baraza hilo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza Bi. Khadija Ngasongwa alisema Mpango Mkakati huo umeandaliwa kwa kuzingatia maono ya Dira ya 2050 ya kuwa na “Uchumi shindani, jumuishi na himilivu unaochochea ustawi wa Watanzania wote”
“Baraza la Wafanyakazi ni jukwaa muhimu la ushirikishwaji. Mpango Mkakati huu tuliojadili ni nyaraka muhimu inayoonesha ramani ya safari ya Tume na unaakisi dhamira yetu ya pamoja ya kuiunga mkono Dira ya 2050 kupitia soko huru, salama kwa mlaji na linalochochea ukuaji wa uchumi shindani ,” alisema Bi. Khadija
Kupitia Azimio la Baraza, watumishi wa FCC wamekubaliana kuunga mkono kikamilifu rasimu ya Mpango Mkakati huo na kushiriki katika utekelezaji wake utakaoanza tarehe 01 Julai, 2026. Maeneo yaliyopewa kipaumbele ni pamoja na kukuza ushindani huru na wa haki, kupambana na bidhaa bandia na kuimarisha ulinzi wa mlaji.
Baraza hilo ambalo hukutana mara mbili kwa mwaka kwa mujibu wa sheria, limeelezwa kuwa chombo muhimu cha kuimarisha mshikamano, uwajibikaji na mawasiliano ya wazi kati ya Menejimenti na Watumishi.
“Kupitia mshikamano huu, tutaongeza ufanisi katika kusimamia ushindani wa haki na kulinda maslahi ya walaji kama sehemu ya mchango wa Tume katika kufanikisha Dira ya Taifa ya 2050,” ilisomeka sehemu ya azimio la baraza.
Uongozi wa Tume umedumisha utamaduni shirikishi katika kujadili masuala ya taasisi kimkakati. Watumishi wote hushirikishwa kupitia ngazi mbalimbali ndani ya Tume kabla ya rasimu kuidhinishwa na Bodi ya Tume ya Ushindani.
FCC itaendelea kuthamini mchango wa Baraza la Wafanyakazi katika maamuzi ya kimkakati sambamba na azma ya kujenga mazingira bora ya kazi na kutoa huduma bora kwa umma.
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
