` KATAMBI ATOA MAMILIONI YA FEDHA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO JIMBONI KWAKE

WANDAMAN HOTEL

KATAMBI ATOA MAMILIONI YA FEDHA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO JIMBONI KWAKE



Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ametoa fedha za mfuko wa Jimbo sh.milioni 61, kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake.
Fedha hizo zimegawanywa kwa Kata zote 17 ambazo zipo Jimbo la Shinyanga Mjini, na kuelekezwa kwenye ununuzi wa vifaa vya ujenzi, ili utekelezwaji wa miradi hiyo ya maendeleo uanze mara moja, kwa ustawi wa wananchi.

Katibu wa Mbunge huyo Samweli Jackson, akizungumza jana kwa niaba yake, wakati wa ziara ya kata kwa kata ili kufuatilia utekelezwaji wa fedha hizo za mfuko wa Jimbo kama zimetumika ipasavyo kununua vifaa vya ujenzi, kwenye miradi ambayo imepagwa na viongozi wa Kata husika kutekelezwa, kwamba Katambi anataka kasi ya maendeleo kwa wananchi wake.
Samweli amesema, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Katambi ametoa fedha za Mfuko wa Jimbo Sh.milioni 61, ili kuchochea kasi maendeleo katika Kata zote 17 Jimboni kwake, kwa kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Ziara ya leo tumefanya ufuatiliaji wa ununuzi wa vifaa vya ujenzi, kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia fedha za mfuko wa Jimbo Kata kwa Kata, na tumetembelea Kata zaidi ya 14, lengo ni kutaka miradi hii, jenzi zake zianze mara moja,” amesema Samweli.
Aidha, amewataka wananchi wa Jimbo hilo, kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Mbunge wao Katambi, ili waendelee kuwatumikia na kuwaletea maendeleo kwa vitendo.

Naye Meya wa Manispaa ya Shinyanga Salum Kitumbo, amempongeza Mbunge Katambi, kwa kuendelea kuguswa na wananchi wa Shinyanga, na kuwapambania kuchochea kasi ya maendeleo, na sasa amegawa fedha za mfuko wa Jimbo katika Kata zote 17 bila ya upendeleo, sababu ya upendo kwao.
Pia, ametoa maelekezo kwa watumishi wa Manispaa hiyo, kwamba vifaa vya ujenzi ambavyo vimenunuliwa kwenye miradi hiyo, kwamba vitumike ipasavyo na kuisimamia yote itekelezwe kwa ubora na thamani ya fedha ionekane.

“kwenye hili nitakuwa mkali, nataka maeneo yote ambayo fedha zinatolewa kwa ajili ya utekelezwaji wa miradi ya maendeleo zisimamiwe kikamilifu, na kusiwepo na ubadhilifu wa aina yoyote, bali zitumike kwa uaminifu mkubwa na kutatua kero za wananchi,” amesema Kitumbo.

Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapindizi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini Said Bwanga, amesema CCM wameridhika na utekelezwaji wa ilani ya CCM kupitia kwa Mbunge Katambi ,sababu wamekuwa wakijionea kwa vitendo utekelezwaji wa miradi ya maendeleo, na kuwaomba wananchi waendelee kukiunga mkono Chama hicho kwa maendeleo zaidi.
Nao Madiwani wamempongeza Katambi kwa kuendelea kutoa fedha kwenye Kata zao, na kuchochea kasi ya maendeleo kwa kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Baadhi ya wananchi wa Shinyanga akiwamo Aghatony Matondo kutoka Ngokolo, wamesema wamefurahi kuona vifaa vya ujenzi kwenye eneo ambalo inataka kujengwa Zahanati ya Kata hiyo, kwamba kilikuwa kilio chao cha muda mrefu kutaka kujengewa Zahanati, lakini sasa Katambi anakwenda kuijenga, wakishirikiana na Diwani wa Kata hiyo Jackline Isaro, na kutatua kero ya ukosefu wa huduma za afya katika Kata hiyo.

Ziara hiyo ya Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga kufuatilia matumizi ya fedha za mfuko wa Jimbo kwenye ununuzi wa vifaa vya ujenzi, waliambatana pia na Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, wakiongozwa na Mchumi Michael Makotwe, ambayo pia itaendelea siku nyingine kwenye Kata zingine ambazo zimesalia.

MAELEZO KATIKA PICHA👇👇
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samweli Jackson akizungumza kwenye ufuatiliaji wa fedha za mfuko wa Jimbo Kata kwa Kata.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mariam Nyangaka anayesghughulikia masuala siasa na mahusiano akizungumza.
Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Said Bwanga akizungumza.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Salum Kitumbo akizungumza.
Mchumi wa Manispaa ya Shinyanga Michael Makotwe, akizungumza.
Ukaguzi wa vifaa vya ujenzi "site" ukiendelea, hapa ni ujenzi wa Zahanati ya Ngokolo.
Ukaguzi wa vifaa vya ujenzi ukiendelea katika Kata mbalimbali Manispaa ya Shinyanga kupitia fedha za mfuko wa jimbo.




Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464