` AMANI MIGODINI YAIMARIKA, WACHIMBAJI WAFANYA KAZI KWA UTULIVU.

WANDAMAN HOTEL

AMANI MIGODINI YAIMARIKA, WACHIMBAJI WAFANYA KAZI KWA UTULIVU.

Wachimbaji mdogo wa madini katika mgodi wa Mwakitolyo uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, wamesema kuwa hali ya amani na usalama migodini imeendelea kuimarika, jambo linalowezesha wachimbaji kufanya kazi zao kwa utulivu na ufanisi zaidi.

Wamesema tofauti na ilivyokuwa hapo awali, kwa sasa wachimbaji wanafanya kazi bila hofu kutokana na kuwepo kwa utaratibu mzuri wa ulinzi na usimamizi wa shughuli za madini.

Mchimbaji mdogo Janeth Ngangula amesema mfumo mzuri uliowekwa na Rais Samia Suluhu Hassan umewezesha amani kuendelea katika migodi na kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ushirikiano na utulivu.

Ameeleza kuwa  kuimarika kwa amani kumechangia kufanya kazi zao kwa uhuru licha ya kuwepo changamoto chache ambazo serikali inaendelea kuzifanyia kazi ili waweze kuendelea kuchangia pato la taifa.

 uzalishaji na kipato kwa wachimbaji wadogo, huku pia kukiwa na ushirikiano mzuri kati ya wachimbaji, viongozi wa eneo husika pamoja na mamlaka zinazosimamia sekta ya madini. 

Janeth amewataka wachimbaji wenzake kuendelea kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ili kudumisha hali hiyo ya utulivu na kuhakikisha sekta ya madini inaendelea kuchangia maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Amesisitiza umuhimu wa kuendeleza juhudi za kulinda amani migodini ili kuhakikisha mazingira salama ya kazi yanadumishwa kwa manufaa ya wote wanaojihusisha na shughuli za uchimbaji.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464