` WAKALA WA MISITU TANZANIA TFS YAGAWA MICHE YA MITI 4,000 NA KUPANDWA WILAYANI KISHAPU

WANDAMAN HOTEL

WAKALA WA MISITU TANZANIA TFS YAGAWA MICHE YA MITI 4,000 NA KUPANDWA WILAYANI KISHAPU

Wakala wa misitu Tanzania TFS kwa kushirikiana na wananchi na wadau wa mazingira Wilayani Kishapu wamepanda miti zaidi ya elfu nne (4,000) katika baadhi ya shule zilizopo katika maeneo ya maeneo ya pembezoni wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali la kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Na Mwandishi wetu kutoka mkoani Shinyanga

Wakala wa Misitu Tanzania TFS, wadau wa mazingira na wananchi wamefanya zoezi hilo kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya misitu Duniani ambapo kiwilaya wamefanya maadhinisho hayo kwa kupanda miti katika maeneo ya shule mbalimbali.

baadhi ya shule za msingi wilayani kishapu zilizopata nafasi ya kushiriki zoezo hilo la upandaji miti ni shule ya msingi bulima na sanjo Shule ya msingi ampapo walimu na wanafunzi wamehimizwa kuitunza miti hiyo ili ikue na kutimiliza malengo ya serikali ili wanafunzi wapate hewa safi, kivuli cha kupumzikia na matunda kwa ajili ya Afya za miili yao.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya misitu duniani, mhifadhi mwandamizi wa misitu wilaya ya Kishapu Tumaini Masatu amesema upandaji huo wa miti unalenga kuikumbusha jamii umuhimu wa kutunza mazingira na kuhakikisha miti hiyo inakua kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Kwa upande wao wadau wa mazingira likiwemo Shirika la TCRS ambalo linajihusisha na utunzaji wa mazingira na elimu ya kilimo cha umwagiliaji wa matone na mafunzo kwa wajasiriamali wametoa elimu juu ya namna bora ya kutunza miti hiyo ili iweze kukua na kuleta tija huku baadhi ya wananchi wakieleza kufurahishwa na hatua hiyo wakisema itasaidia kuboresha mazingira na hali ya hewa katika eneo hilo.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Nicolaus Masindi amewataka walimu katika shule zilizopandwa miti hiyo kuhakikisha wanasimamia utunzaji wake ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.



👉👉👉👉








Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464